Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe. Ussi Salum Pondeza (AMJAD) Apiga Jeki Kamati ya Central League Wilaya ya Mjini

Zawadi za Vikombo kwa Washindi wa Michuano wa Ligi ya Watoto Central League Wilaya Mjini Unguja, vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) Kwa washindi wa ligi hiyo kwa mwaka huu 2016/2017 kuazia ngazi za Junior, Central na Juvounal watakabidhiwa zawdi hizo wakati wa michezo yao ya mwisho leo katika viwanja vya Amaan Zanzibar. 
Katibu wa Central League Wilaya ya Mjini Unguja Ndg. Alawi Haidar akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa zawadi za washindi wa Ligi za Watoto Wilaya ya Mjini Unguja, zilizotolewa na Mbunge wa Chumbuni Zanzibar na Mlezo wa Mashindano hayo Mhe Ussi Salum Pondeza. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akimkabidhi Kombe Mwenyekiti wa Kamati ya Central League Wilaya ya Mjini Unguja Ndg. Khamis Machano, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akimkabidhi Kombe Mwenyekiti wa Kamati ya Central League Wilaya ya Mjini Unguja Ndg. Khamis Machano, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar. kushoto kwa Mbunge ni Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Miraji Khamis Mussa.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza (AMJAD) kushoto kwa Mbunge Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe Miraj Khamis Mussa na Katibu wa Central Wilaya ya Mjini Unguja Ndg Alawi Haidari na kulia Mwenyekiti wa Central League Ndg Khamis Machano wakiwa za Vikombe vya Washindi baada ya kukabidhiwa na Mhe Mbunge AMJAD.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Zanzibar Mhe, Ussi Salum Pondeza (AMJAD) akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar baada ya kukabidhi zawadi kwa Viongozi wa Ligi za Watoto Wilaya ya Mjini Unguja katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mwandishi wa Michezo wa Redio Bahari FM akiwa makini kufuatilia hafla hiyo.
Mwandishi wa habari za michezi wa Redio Chuchu FM Zanzibar akimsikiliza Mbunge wa Chumbuni wakati akizungumza katika hafla hiyo.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.