Habari za Punde

Mchango wa kuwafutarisha na kuwapatia Eid ya furaha mayatima Zanzibar

Baadhi ya watoto mayatima wakifutarishwa katika Ramadhani ya mwaka jana hapa Zanzibar


Ndugu Wapendwa,
Sote tunaifahamu hali ya maisha duni wanayopambana nayo baadhi ya watoto mayatima kule Zanzibar. Hatuwezi kuibadilisha hali yao hio, lakini tunaweza angalau siku moja kuwafutarisha vizuri katika hii Ramadhani ijayo na kuwapa mkono wa Eid siku ya Sikukuu.
Kwahivyo, ZANZIBAR-CANADIAN DIASPORA ASSOCIATION (ZACADIA) ya Toronto, Canada, inatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoishi nje kuungana pamoja ili kuwafutarisha watoto hao mayatima na kuwapa mkono wa Eid siku ya Sikukuu.
Kama unaguswa na hali ya mayatima kule Zanzibar basi changia chochote unachokiweza ili watoto hao mayatima wafutari vizuri angalau hio siku moja katika Ramadhani ijayo na siku ya Sikukuu wapate mkono wa Idi.
Tafadhali changia and Allah will reward you, Inshaa Allah!
Kampeni itamalizika Ramadhani ya 10, ili kabla Ramadhani haijesha tupate muda wa matayarisho ya shughuli ya kufutarisha hao mayatima kule Zanzibar na pia kupata muda wa kuwanunulia nguo za Sikukuu, kwani hali zao kama mnavyoona pichani hapa juu ni taabani
Tuma mchango wako kwa muwakilishi aliekuwepo karibu na wewe:
CANADA:
Hassan Othman @+1.647.404.8618 (Toronto)
Bi Shahida Hamad @+1.289.696.3089 (Toronto)
U. S. A
Mohammed Masoud @1.330.880.9524 (Ohio)
UNITED KINGDOM:
Miss Fauzia Karama @+44.7847.024.456 (Manchester)
Abdalla Juma (Dulla Ndende) @ +44.7909.225.287 (Milton Keynes)
EUROPE:
Dr. Muhammed Mwinyi Khamis @ +46.70.426.9707 (Scandinavia / Sweden)
Nabil Salum (Nasser) / NASMO @ +32.487.28.39.96 (Belgium)
MIDDLE EAST:
Mohamed Omar @ +971.50.424.6878 (Dubai, U.A.E)
Ali Said Ali @+968.9.509.7454 (Muscat, Oman)
FAR EAST:
Suleiman Ali Al Rawahy @+81.80.4027.3510 (Japan)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.