Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Akabidhi Vifaa kwa Wananchi Wanaokaa katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wa Kambi hiyo ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Bi Rahma Kassim Ali wakati alipofika kuwatembelea Wananchi hao na kuwafariji kwa maafa yaliowakuta na kukabidhi misaada ya vifaa mbalimbali kambini hapo. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Mkuu wa Kambi hiyo Bi Rahma Kassim Ali akiwatembelea Wananchi wanaoishi kambi hiyo kwa kuwafariji na kukabidhi msaada kwao.
Mama Mwanamwema Shein akitembelea Kambi hiyo Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja Wilaya ya Magharibi B. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Ali Juma, akitowa maelezo ya maendeleo ya Kambi hiyo, wakati alipofika kuwatembelea na kuwafariji.
za masika.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kambi hiyo Bi Rahma Kassim Ali, akipofika kambini hapo kuwatembelea Wananchi hao na kuwafariji na kukabidhi misaada ya vifaa mbalimbali kwa mahitaji yao.  
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitikia dua iliyokuwa ikisomwa na mmoja wa watoto wanaoishi katika kambi hiyo wakiwa katika madrasa wakijisomea kambini hapo Skuli ya Mwanakwerekwe C Wilaya ya Magharibi Unguja.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, na Ujumbe wa Maofisa wa Kampuni ya ZTE, wakiitikia dua iliokuwa ikisomwa na mmoja wa Watoto wa Kambi hiyo, wakati alipofika kuwatembelea na kuwafariji.


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wananchi wanaoishi katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C, kutokana na makaazi yao kujaa maji wakati wa mvua za masika zilizonyesha hivi karibuni.kulia Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar Bi Wu Yan, na kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif.
Baadhi ya Wananchi wanaoishi katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akitowa nasaha zake na kuwafariji kwa maafa ya mvua za masika na kuleta madhara katika makaazi yao.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi msaada wa madaftari Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Joseph Meza, kwa ajili ya Watoto wa Familia zilizopata maafa ya mvua za masika.

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi msaada wa vyandarua Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Joseph Meza, kwa ajili ya Wananchi waliopata maafa ya mvua za masika.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimsikiliza mmoja wa Mwananchi Maryam Maulid,anayeishi katika Kambi hiyo akitowa shukrani kwa Mama Mwanamwema Shein, kwa ujio wake na kukabidhi misaada kwao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.