AL-IHSAAN GIRLS SECONDARY SCHOOL
RISALA YA MAHAFALI YA TATU YA WANAFUNZI WA KIDATO
CHA SITA 2016
MHESHIMIWA
MGENI RASMIN. WAZIRI WA `BIASHARA, VIWAANDA NA MASOKO, BALOZI AMINA SALUM ALI.
MHESHIMIWA
BALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA, MR JASSEM IBRAHIM AL – NAJIM
NDUGU
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA AFRICA MUSLIM AGENCY MR. AIMAN MOH’D
MWENYEKITI
WA KAMATI YA SKULI, NDUGU VUAI MUSSA.
MWALIMU
MKUU WA SKULI YA AL-IHSAAN, NDUGU
ABUBAKAR AHMAD MWADINI.
NDUGU
MAAFISA WA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
NDUGU
VIONGOZI WA ZAPS
MHESHIMIWA
MWAKILISHI WA JIMBO LA M/KWE
WAHESHIMIWA
MASHEHA NA MADIWANI WA WADI NA SHEHIA ZA MWANAKWEREKWE NA MAGOGONI.
WAGENI
WAALIKWA,
NDUGU
WANAFUNZI
MABIBI
NA MABWANA ITIFAKI INAZINGATIWA
Asalamu
alykum Warahmatullah Wabarakatuh
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Awali
ya yote, napenda kumshukuru allah (S.W) kwa kutujaalia uhai na uzima kwa
kutuwezesha kukutana hapa katika siku hii ya leo.
Pili,
kwa niaba ya walimu na wanafunzi wenzangu naomba nitumie nafasihii kukushukuru
wewe mgen rasmin, kwa kukubali kushirikiana nasi katika mahafali yetu ya tatu
ya kidato cha sita.
Licha
ya majukumu yako mazito ya kitaifa, hii inazihirisha wazi kwamba upo pamoja
nasi kukamilisha sherehe hizi hasa kwa nafasi yako ya kitaifa wewe ni mlezi na
kwetu ni kiongozi wa wizara ya biashara, viwanda na masoko, aidha tunapenda
kutumia nafasi hii kuwashukuru wazazi wetu kwa mahudhurio yao.
Muheshimiwa
mgeni rasmin.
Kihistoria,
skuli hii ya wasichana imeanzishwa na shirika Afrika Muslim Agency, February
2002 ikiwa na madarasa manane, vyumba viwili vya walimu, ofisi ya mwalimu mkuu,
maabara moja, chumba cha maktaba, chumba cha chai na vyoo ishirini na sita
(26). Na mwalimu mkuu wa mwanzo, alikua marehemu Bi Maryam Omar Moh’d, ambaye aliongoza skuli kwa takriban miaka
saba (7).
Shule
ilianza na jumla ya wanafunzi 89 wa kidato cha kwanza na walimu sita (6),
katika kipindi cha uongozi wake, marehemu Bi Maryam alisisitiza sana suala la
nidhamu ya wanafunzi kwa wanafunzi, walimu kwa walimu na baina ya walimu na
wanafunzi. Aidha, mafanikio ya jitihada zake yalionekana baada ya kipindi
kifupi ambapo wanafunzi wa mwanzo waliofanya mitihani ya taifa kidato cha nne
mwaka 2005 na mwaka 2007, kufikia asilimia mia matokeo yao, matunda ya jitihada
zake, busara na hekima zake baada ya kipindi kifupi cha uongozi wake nabado
matokeo mazuri yanaendelea kupatikana hadi sasa sio tu kwa masomo lakini pia
kitabia za walimu na wanafunzi.
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Kuanzia
mwaka 2005 hadi mwaka 2015, shule imetoa wahitimu 554 wa kidato cha nne, ambapo
548 walifaulu na kupata vyeti, sawa na silimia 98.91, aidha kati ya wanafunzi
548 waliopata vyeti, wanafunzi 296 wamefaulu kuendelea kidato cha tano na sita,
hii ni sawa na asilimia 54.01. mafanikio haya yamepelekea wazazi na wanafunzi
kuleta watoto wao kwa wingi, hivi sasa shule ina jumla ya wanafunzi 450 na
walimu 25 kati yao wanawake 9 na wanaume 16
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Jengo
jipya liliopo upande wa kulia la madarasa sita na maabara mbili, limewezesha
kuanzishwa kidato cha tano na sita kuanzia mwaka 2012 hii ni pamoja na
ongezeko la vifaaa vya maabara ambavyo
shirika linagharamia, vilevile kwa sasa shule haina upungufu wa vikalio nikiwa
na maana viti, meza na madawati.
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Kwa
upande wa kidato cha tano na sita, hadi kufikia mwaka 2016, shule imeshatoa
wanafunzi 88 kwa mikupuo mitatu. Kwa mkupuo wa mwanzo mwaka 2012-2014 kati ya
wanafunzi 20 waliofanya mitihani ya kidato cha sita ya mwaka 2014 wanafunzi 19,
sawa na asilimia 95 walifaulu na kupata vyeti vya kidato cha sita na wamejiunga
na vyuo vikuu mbali mbali nchini. Mwaka 2015 idadi ya watahiniwa walikua 21,
ambapo jumla ya wanafunzi 20 walifaulu na kujiunga na vyuo mbali mbali na kwa
mwaka huu tupo jumla ya wahitimu 47 ambao wapo mbele yako na kwa sasa
tunasubiri matokeo yetu ili tujiunge na vyuo mbali mbali biidhini llah.
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Kama
hayo hayatoshi Shirika linadhamini wanafunzi wote wanaojiunga na kidato cha
tano na sita ndani ya skuli yetu kwa wale wanaofaulu kwa ngazi ya daraja la
kwanza na la pili katika mitihani ya “O” level kudhaminiwa masomo ya juu advance, hii inatupa faraja
sisi wanafunzi na inatia moyo na kutupa ari sisi wanafunzi kuongeza bidii ili
kunufaika na fursa hii adhimu na ya ghali.
Pamoja na ufadhili huo pia shirika linaendeleza ufadhili wa kuwafadhili
sare za skuli kwa wanafunzi yatima na wenye hali ngumu. Aidha tunapenda
kulishukuru na kulipa pongezi shirika la Africa Muslims Agency kwa kuongeza
nguvu ya msaada wa chakula kwenye maandalizi ya mitihani yetu.
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Fursa
nyengine ambayo wanafunzi wanaipata wanaofaulu na kuwa na sifa za kujiunga vyuo
wanapeewa fursa nyengine ya kudhaminiwa masomo yao ya juu.
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Penye
mafanikio hapakosi changamoto, katika maisha yetu ya kidato cha kwanza hadi cha
sita tumekabiliwa na changamoto tatu kuu, kwanza kukosa dahalia ambapo
wanafunzi wanaweza kuishi kwa muda wote ili kuwawezesha wanafunzi kujisomea kwa
muda wote, uzowefu unaonesha kwamba shule nyingi zenye dahalia O level na
advance matokeo yao yanakua mazuri ukilinganisha na zile ambazo hazina dahalia,
pili, uwezo mdogo wa wazazi wa kuchangia huduma za chakula, tatizo hili
limepelekea wanafunzi kukaa muda mdogo kambini, tatu, tatizo la mara kwa mara
la kuharibika kwa miundombinu ya maji.
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Tunatoa
shukurani za dhati kwa Mwalimu mkuu maalimu Abuu Bakar Ahmad na viongozi
wenzake kwa jitihada zao na moyo wao wa kuongoza skuli kwa hekima na busara
ambazo zimesaidia kutatua changamoto mbali mbali siku hadi siku. Aidha
tunawashukuru walimu wetu wa masomo kwa juhudi zao za kutupa taaluuma pamoja na
malezi mazuri.
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Vile
vile tunatoa shukurani zetu kwa mwalimu mkuu mstaafu mwalimu Ibrahim Marine kwa
uongozi wake wa busara na hekima tangu mwaka 2009-2015, pia tunamshukuru mlezi
wetu na mshauri wetu wa skuli mama yetu Bi Mgeni Moh’d Said, bila ya kusahau
uongozi wa skuli wakiwemo Bi Yusra Juma, Maalimu Omar Halfan, Maalim Rashid Dadi
na Maalim Abdallah Nassor kwa kuwa nasi bega kwa bega kipindi chote cha kambi
tulichokuwepo hapa skuli
Mheshimiwa
mgeni rasmin.
Tunaomba
utukubalie tena shukurani zetu na tunakushukuru kwa kuwacha kazi zako na kujumuika
nasi.
Mwisho
tunamuomba Allah atupe kila la kheri wewe na sisi pamoja na walimu wetu na
wazazi wetu na wanafunzi wenzangu. AAMIN
Ahsanteni
kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment