Habari za Punde

Balozi Seif atoa misaada jimboni kwake

 Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Madeski 50 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pembe Juma kwa ajili ya Skuli ya Msingi ya Mahonda, hafla iliyofanyika kwenye skuli hiyo.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Riziki Pemba Juma akimkabidhi Madeski 50 Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi ya Mahonda Mwalimu Kazima Moh’d Makame.
 Baadhi ya Madeski yaliyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi yenye thamani ya shilingi Milioni 8,500,000/- akitekeleza ahadi aliyotowa wiki chache zilizopita.

 Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya Upishi Mwenyekiti wa Kikundi cha Utamaduni cha Akina Mama wa Kijiji cha Kichungwani  Bibi Mwema Jumanne ili kuendeleza miradi yao ya kujitegemea.

 Balozi Seif akikabidhi fedha kwa Katibu wa CCM Tawi la Zingwe zingwe Nd. Abdulrahman Hassan kwa ajili ya kukamilisha kazi za upigaji plasta wa Tawi lao.

 Balozi Seif akimkabidhi fedha taslim Mwenyekiti wa Tawi la CCM Zingwe zingwe Nd. Omar Juma Omar ajili ya ujenzi wa Mnara wa kuwekea Tangi la Maji safi la Skuli ya Msingi ya Zingwe zingwe.
  Balozi Seif  akimkabidhi fedha Taslim Imam wa Msikiti wa Ijumaa Mahonda kwa ajili ya Shughuli za Tahfidh Quran kwenye kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Balozi Seif akimkabidhi fedha taslim Mwalimu wa Madrasatul Laaila – hailallah ya Kijiji cha Kitope kwa ajili ya kuendeleza harakati za Madrasa hiyo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.