Habari za Punde

Cheki Tanzania yazindua huduma ya kutoa magari bandarini kwa wanunuzi wa magari nchini

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Cheki Tanzania, Mori Bencus akielezea kuhusu huduma ya uunganishwaji wa uagizaji magari kutoka nje ya nchi na huduma ya utoaji wa magari bandarini (clearing and forwarding), huduma ambayo kampuni yake imeanza kuitoa kwa Watanzania wanaoagiza magari.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiendelea na kazi yao ya kuchukua taarifa kwa ajili ya kuupasha umma kuhusu huduma ya clearing and forwading ambayo inatolewa.Mtandao wa kuuza magari mtandaoni wa Cheki.co.tz umezindua huduma mpya ya uunganishwaji wa uigizaji magari kutoka nje ya nchi na huduma ya utoaji magari bandarini (clearing and forwarding), huduma ambayo itawarahisishia wananchi ambao wanaagiza magari nje ya nchi kuwa na uhakika wa usalama wa magari wanayoagiza mpaka yanakapowafikia.
Akielezea huduma hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Cheki Tanzania, Mori Bencus, alisema kampuni yake imeanzisha huduma hiyo ili kuwarahisishia Watanzania wanaoanzisha magari nje ya nchi kutokana na kubaini kuwa wamekuwa wakisumbuka kukamilisha uagizwaji wa magari na kuyatoa bandarini.
“Tayari tumewapa wateja wetu chaguo kubwa la magari kutoka kwa wauzaji wa kuaminika kutoka nje ya huduma hii ya utoaji wa mizigo itarahisisha utoaji wa magari kutoka bandarini na hivyo wateja kupunguza gharama na muda wa kusubiri,” alisema Bencus.
Nae Kaimu Meneja Masoko wa Cheki Tanzania, Juliana Ntemo, alisema kuwa kampuni hiyo haihusiki na uuzaji wa magari ila inachofanya ni kumuunganisha mnunuzi wa gari na muuzaji ili waweze kufanya biashara kwa haraka na urahisi zaidi.
Ujio wa huduma hiyo imekuwa mwendelezo wa uboreshwaji wa huduma za ununuzi wa magari kwa kupitia mtandaoni ambazo zinafanywa na mtandao wa Cheki.co.tz ambao unafanya kazi na wauzaji wa magari wa kimataifa wa  nje ya nchi na wauzaji wa magari wa hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.