Habari za Punde

Mkutano wa ZSTC na Wakulima wa zao la Karafuu - mwisho wa msimu

 WAKULIMA wa Karafuu kutoka Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, wakifuatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano maalumu ulioandaliwa na ZSTC kwa wakulima wake kila mwisho wa msimu wa zao la karauu.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MWENYEKITI wa Bodi ya shirika la biashara la taifa ZSTC Zanzibar, Mwalimu Suleiman Kassim, akizungumza na wakulima wa karafuu Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba. .(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MAAFISA mbali mbali wa vikozi vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakiongozwa na kamanda wa Polisi Mkoa huo Hassan Nassir Ali wa kwanza kutoka kushoto, wakifuatia mkutano wa kulima wa ZSTC Wilaya ya Micheweni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe:Omar Khamis Othamni, akizungumza na wakulima wa karafuu wilaya ya Micheweni katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la ZSTC, huko katika skuli ya Michweni Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 AFISA masoko kutoka shirika la biashara la taifa ZSTC Salum Abdalla Kibe, akiwasilisha mada ya Tathmini ya utekelezaji wa kazi kwa msimu wa vuno la karafuu 2015/2016 kwa wakulima wa zao hilo huko katika skuli ya Micheweni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 SHEHA wa Shehia ya Micheweni mjini Dawa Juma Mshindo, akichangia katika mkutano wa wakulima wa zao la Karafuu wa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali, akichangia mada katika mkutano wa wakulima wa Wilaya hiyo, uliondaliwa na shirika la biashara la ZSTC.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 AFISA mdhamini wa Shirika la Biashara la Taifa ZSTC Pemba, Abdalla Ali Ussi akijibu michengo mbali mbali iliyotolewa na wakulima wa karafuu kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKULIMA bora wa zao la karafuu Wilaya ya Micheweni 2015/2016 Abdalla Saidi Abdalla, akikabidhiwa cheti chake na Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Omar Khamis Othaman, huko katika mkutano wa wakulima wa zao hilo huko Micheweni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKULIMA bora wa kwanza Wilaya ya Micheweni wa zao la Karafuu 2015/2016 Seif Abdalla Seif, akikabidhiwa cheti chake na Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Omar Khamis Othaman huko katika mkutano wa Wakulima wa zao hilo huko Micheweni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.