Habari za Punde

Ziara ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Ndg Shaka Mkoani Singida.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg:Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Puma ilioko Wilaya ya Ikugi akiwa katika ziara kikazi kuimarisha Chama na Jumuiya zake Mkoani Singida .
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Puma Wilayani Ikugi wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu UVCCM  Ndg:Shaka Hamdu Shaka, wakati akiwa katika ziara yake ya Kikazi Mkoani Singida.
 Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Mariam Gwau akizungumza kero na changamoto zinazo wakabili Shuleni kwako.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM TAIFA Ndg:Shaka Hamdu Shaka pamoja  na Msafara alio ambatana nao akizungumza na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mohamed Nkya. 
Na Fahadi Siraji :Singida 
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi umeitaka halmashauri ya wilaya ya Ikungi kutenga bajeti ya dharura itakayofanikisha mradi wa maji safi kufika katika shule ya sekondari Puma iliopo wilaya Ikungi Mashariki.


Aidha Umoja huo umeisisitiza halmashauri hiyo katika upangaji wa bajeti zake kuyapa kipaumbele masuala ya msingi ambayo ni muhimu kwa maisha ya jamii.  

Katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya sekondari hiyo,mwanafunzi Mariam Gwau anayesoma kidato cha nne alielezea tatizo la barabara na umbali toka mahali wanakoishi hadi kufika  shuleni  ni hatarishi kwao kiusalama


Pia alisema kukosekana kwa maji safi na salama kwao ni shida inayowapa msongo wa mawazo kwasababu wanateka maji machafu katika bwawa moja wakichangia na mifugo.


"Mimi na wanafunzi wenzangu sasa tunakaribia kumaliza  masomo yetu ili tufanye mtihani wa kuelekea kidato cha tano, tuna mwaka mmoja sasa hatujafundishwa somo la fizikia, kwetu hii sawa na kutukatisha tamaa kwa maendeleo ya elimu "Alisema Maryam 

Mwanafunzi mwingine anayesoma wa kidato cha tatu Angelina Amani alimueleza kaimu katibu mkuu Shaka Hamdu Shaka kuwa shuleni hapo hapana umeme, maabara haijamalizika pia haina vifaa vya kufundishia kwa vitendo jambo hilo pia akidai linawasikitisha sana na kuwa kikwazo kikubwa katika Masomo yao .


Akijibu hoja hizo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Abel Sury alisema upo mradi wa maji safi lakini kwa mwaka wa fedha 2016 /2017 mpango wa kufikisha maji katika  shule hiyo  haupo pia jengo la maabara likifikia hatua ya linta halmashauri itasaidia.


Matamshi hayo ya Makamu Mwenyekiti hayakuonekana kumridhisha Shaka ambaye alimtaka Makamu huyo Mwenyekiti kuhakikisha maji yanafika sekondari Puma haraka ndipo alipoamua kwenda  kuonana na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo. 

Alipozungumza na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mohamed Nkya ofisini kwake alimisitiza kutenga bajeti ya dharura na kufikisha maji safi katika shule hiyo. 


Shaka alimulekeza Mkurugenzi huyo kuwa masuala yanayohusu huduma za jamii zinapaswa kuwekewa muhimu na kupatiwa suluhisho la kudumu kabla hayajawa majipu na kero zinazokatisha juhudi za wananchi hasa wanafunzi wanaotakiwa kupata elimu bora. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.