Habari za Punde

Siku Ujumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China Jimbo la Jiangsu Ulipowasili Zanzibar kwa Ziara ya Siku Mbili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Gavu. akijiandaa kuupokea Ujumbe wa Chama cha Kikomunist cha China wakati kilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya Siku mbili Zanzibar. 
Ujumbe wa Serikali na Chama Ukiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Gavu, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai na Meya wa Mji wa Zanzibar Khatib Abdraham Khatib wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuupokea ujumbe huo.
Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu Bw.Luo Zhijon, akivishwa maua baada ya kuwqasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, akivishwa maua na Mtoto Naifat Fouz baada kuwasili Zanzibar kwa ziara ya siku mbili. 
Katibu wa Chama cha Kikoministi cha China kutoka Kamati ya Jimbo la Jiangsu,  Bw.Luo Zhijon, akimsalimia mtoto Naifat Fouz baada ya kumvisha shada la maua.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.