Habari za Punde

Zantel yatoa milioni 10 kwa Jumuiya ya Wakulima wa Mwani Zanzibar


Waziri wa Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Maudline Cyrus Castico, akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel Bwana Benoit Janin,  wakati akiwasili katika majengo ya Zantel Amani Zanzibar kuhudhuria hafla ya kuwakabidhi Hundi Jumuiya ya Wakulima wa Mwani Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Maudline Cyrus Castico, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel na Makamu wa Rais Mambo ya Nje wa Millicom Bi Rachel Samren, alipowasili katika Afisi za Zantel Amani Zanzibar. 
Afasi wa Kampuni ya Simu ya Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akitowa maelezo kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya Jumuiya ya Mwani Zanzibar kusainia kununulia Vifaa vya Kilimo hicho.  
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel Bwana Benoit Janin, akizngumzia msaada huo kwa ajili ya Jumuiya ya Wakulima wa Mawazi Zanzibar amesema kuhakikisha wakulima wa mwani wanaendelea na jitihada zao katika kilimo hicho.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel na Makamu wa Rais Mambo ya Nje wa Millicom Bi Rachel Samren, amesema imani yetu kama Zantel ni kuwawezesha wanawake ni jambo muhimu na sahihi la kufanya kwa sababu mwanamke ndiye nguzo ya jamiikatika uchumi wa mwanake.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel na Makamu wa Rais Mambo ya Nje wa Millicom Bi Rachel Samren, akimkabidhi mfano wa hundi,Waziri wa Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Maudline Cyrus Castico kwa ajili ya Wakulima wa Mwani Zanzibar kununulia Vifaa vya zao hilo kwa Wakulima hamo, hafla hiyo imefanyika katika Afisi za Zantel Amani Zanzibar. 
Waziri wa Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Maudline Cyrus Castico,akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi hundi kwa jumuiya ya wakulima wa Mwani Zanzibar iliotolewa na Kampuni ya Simu ya Zantel kwa ajili ya kununulia Vifaa vya kilimo cha Mwani Zanzibar, kwa wana Jumuiya hiyo kuimarisha zao hilo.  
Viongozi wa Jumuiya ya Wakulima wa Mwani Zanzibar wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa hundi na Kampuni ya Simu ya Zantel.
Wafanyakazi wa Zantel Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhiwa Hundi Wakulima wa Mwani Zanzibar.
Maofisa wa Zantel Amani Zanzibar wakiwa katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima wa Mwani Zanzibar Bi Pavu Mcha Khamis akitowa shukrani kwa kampuni ya Simu ya Zatel kwa msaada wao shilingi milioni kumi kusaidia kilimo hicho kwa kununulia Vifaa vya Zao hilo. Na kusema kilimo chao kina changamoto kwa kipindi kirefu tumekuwa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali za upatikanaji wa vifaa vya kilimo pamoja  na fursa ya masoko.
Waziri wa Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Mhe Maudline Cyrus Castico akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Zanztel na Wakulima wa Mwani Zanzibar kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel na Makamu wa Rais Mambo ya Nje wa Millicom Bi Rachel Samren na kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel Bwana Benoit Janin,   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.