WANANCHI wa shehia ya Mgagadu Jimbo la Chambani,
wilaya ya Mkoani Pemba, waliohudhuria mkutano wa kupokea msaada wa kisheria
bila ya malipo, kutoka kwa watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar
ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mipango wa Kiuto cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed, akifafanua jinsi wanavyotoa
msaada wa kisheria bila ya malipo, wakati watendaji wa Kituo hicho na baadhi ya
wanasheria, walipofika shehia ya Mgagadu wilaya ya Mkoani kutoa msaada huo, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
NAIBU sheha wa shehia ya Mgagadu Kassim Juma Makame,
akifungua mkutano maalumu wa kutoa msaada wa kisheria, kwa wananchi wake,
ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia
ni Naibu Mwenyekiti wa mahakama ya ardhi Chakechake, Pemba Salim Hassan Bakar na
kushoto ni Mratib wa ZLSC Pemba Fatma Khamis Hemed,(Picha na Haji Nassor, Pemba).
MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC
tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akifafanua kuhusu kosa la ubakaji kisheria,
kwenye mkutano wa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa shehia ya Mgagadu
wilaya ya Mkoani Pemba, katikati ni Naibu sheha wa shehia ya Mgagadu Kassim
Juma Makame na kulia ni Naibu Mwenyekiti wa mahama ya ardhi Chakechake Pemba
Salim Hassan Bakar, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MWANAFUNZI wa skuli ya Mizingani wilaya ya Mkoani
Pemba, Rashid Omar Mohamed akitaka ufafanuzi wa kuchelewa kwa kesi za ubakaji, kwenye
mkutano wa msaada wa kisheria, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba na kufanyika shehiani humo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment