Habari za Punde

Ligi yaUjerumani Bundesliga kutangazwa moja kwa moja kwa Kiswahili


Kuanzia Agosti 27, 2016, wachambuzi wetu watakuletea moja kwa moja mechi moja kupitia redio katika lugha ya Kiswahili. Hayo ni makubaliano yaliyofikiwa kati ya Ligi ya Soka Ujerumani (DFL) na shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani DW.

DW inaitikia shauku kubwa iliyoonyeshwa na mashabiki wa soka Afrika wanaofuatilia ligi ya Ujerumani ambayo ina wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani iliyoshinda kombe la dunia na pia wachezaji kutoka barani Afrika. 

Kwa kutoa uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili inayozungumzwa na watu wengi katika kanda ya maziwa makuu, DW itawafikia wasikilizaji nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Uchambuzi wa kwenye redio ni nyongeza ya matangazo ya Bundesliga yanayorushwa na StarTimes ambayo ni mshirika wa DFL katika eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Kupitia huduma hii, DW inapanua matangazo yake ya michezo kwani wanahabari wawili kutoka idhaa ya Kiswahil, kila Jumamosi watachambua mechi moja katika matangazo ya moja kwa moja. 

Katika muda wa matangazo unaoanza saa 9:25 mchana hadi saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, DW itawaletea wasikilizaji wa Afrika Mashariki habari za kina na matokeo ya mechi nyingine za siku hiyo.

Vipindi vya redio vya DW vinapendwa sana katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara. DW, ambayo ni shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani, inawafikia wasikilizaji wengi kupitia idhaa zake za Kiswahili, Hausa, Amharic, Kifaransa, Kiingereza na Kireno. 

Vipindi vinasambazwa kupitia mamia ya redio washirika za FM na kupitia masafa mafupi na redio ya satelaiti. Watu wapatao milioni 40 husikiliza vipindi vya redio vya DW mara kwa mara, hasa kwa lugha ya Kiswahili.

“Huduma ya DW kutangaza mechi za DFL ni ushindi kwa kila mtu. Deutsche Welle italifikia kundi makhsusi la mashabiki wa kandanda na kuwafanya watu wavutiwe na Bundesliga katika mataifa ambako redio inatoa mchango mkubwa,“ amesema Mkurugenzi Mtendaji wa DW, Peter Limbourg. 

Washirika wa DW ambao wako nje ya eneo linalofikiwa na matangazo ya redio ya Kiswahili wameonyesha shauku pia.
Watumiaji wa DW wanaweza pia kupata taarifa kuhusu soka la Ujerumani katika mtandao na kwa lugha mbalimbali. Habari za Kiingereza zinapatikana dw.com/bundesliga

Kwenye televisheni, kipindi cha “Kick off!” kinakuletea uchambuzi wa Bundesliga mara mbili kwa wiki. Tarehe 5 Septemba, “Kick off!” itaonyesha pia filamu maalumu kuhusu nguli wa Bundesliga kutoka Afrika, Pablo Thiam na Anthony Baffoe, ambao ni wanasoka wawili wa kipekee wenye historia tofauti kabisaa za kikazi na kimaisha.

Andrea Schmidt 
Leiterin Kisuaheli
Head of Kiswahili Departement
Swahili

Deutsche Welle (DW)
Kurt-Schumacher-Str. 3
53113 Bonn
Germany

+49.228.429-4903
+49.228.429-4900
+49.172.2618323
andrea.schmidt@dw.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.