Habari za Punde

Maziko ya mwandishi wa habari wa Redio Jamii, Mkoani Pemba

Mwandishi Seif Hassan enzi za uhai wake

 MAMIA ya wananchi, Waandishi wa habari wakiwa wameubeba mwili wa Marehemu mwandishi wa Habari wa Radio Jamii Mkoani na Mwanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Time School and Journalism (TSJ)Tawi la Pemba, Seif Hassan Mohamed kuupeleka katika makazi yake ya Mwisho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 WAUMINI mbali mbali wa Dini ya Kiislamu wakimswalia Marehemu Seif Hassan Mohamed, aliyefariki dunia baada ya kupata ajali jana majira ya saa moja na nusu usiku huko Mkoani(Picha na Haji Nassor, PEMBA.)
 SHEKH Salmin Sheha Ussi, akiwaongoza wananchi katika mazishi ya Mwandishi wa habari wa Radio Jamii Mkoani Seif Hassan Mohamed, aliyefariki dunia jana usiku na kuzikwa kijijini kwao Stahabu Mkanyageni Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


 WANANCHI mbali mbali Kisiwani Pemba wakifukia kwa mikono kaburi la Mwandishi wa Habari wa Radio Jamii Mkoani Sif Hassan Mohamed, aliyefariki dunia jana Usiku na kuzikwa huko kijijini kwao Stahabu Mkanyageni Wilaya ya Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.