Spika
wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir
Ali Maulid yuko nchini Mauritius kuhudhuria Mkutano wa 47 wa Umoja wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afirika (CPA African Region).
Mkutano
huo ulioanza Ogasti 22 na kutarajiwa kumalizika Ogasti 27 unafanyika katika
hoteli ya Intercontinental Balaclava Mauritius ambapo unahudhuriwa na washiriki wapatao 400 kutoka nchi wanachama 20, chini ya mwenyeji wao Spika wa nchi hiyo Bibi Santi
Bhai Hanoomajee ambae kwa sasa ndie Rais wa Jumuiya hiyo kikanda.
Tanzania,
Afrika ya Kusini , Msumbiji, Uganda na
Kenya ni miongoni mwa nchi zinazoshikiriki katika mkutano huo
ambapo pamoja na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid, mshiriki mwengine kutoka Zanzibar ni
Mwakilishi wa Tunguu Mheshimiwa Simai Mohammed Mpakabasi .
Miongoni
mwa mada zinazojadiliwa katika mkutano
huo ni pamoja na Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ikiwa ni miongoni mwa mkakati
wa kupunguza umasikini pamoja na nafasi ya
Mabunge katika kudumisha haki,
amani na ushiriki mzuri wa jamii katika
shughuli za kisiasa.
Mada
nyengine zinazozozungumzwa ni ustawi wa jamii
kiafya, kimazingira na kielimu pamoja namaendeleo ya vijana na kuichumi miongoni mwa nchi wanachama.
Awali
Mheshimiwa Spika Zubeir na Mheshimiwa Simai Mpakabasi walihudhuria Mkutano wa Kamati Tendaji ambao ulipitia agenda mbali mbali za Mkutano
Mkuu.
Zanzibar
ni mwanachama wa CPA African Region,
ambapo Baraza la Wawakilishi limekua
likishiriki mara kadhaa katika mikutano, semina na mafunzo
yanayoandaliwa na jumuiya hiyo.
Imetolewa
na
Divisheni ya Uhusiano,
Baraza la Wawakilishi,
Zanzibar.
August 25, 2016
No comments:
Post a Comment