Habari za Punde

Tafrija ya Kumkaribisha Balozi Mdogo wa China Nchini Zanzibar

Balozi Mdogo wa China Nchini Zanzibar Balozi Xie Xiuowu, akihutubia wakati wa kujitambulisha katika chakula maalum kilichoandaliwa na Ubalozi wa China Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud Mohammed, akihutubia wakati wa hafla ya kumkaribisha Balozi Mdogo Mpya wa China Zanzibar Balozi Xie Xiuowu, hafla hiyo imeandaliwa na Ubalozi wa China Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

Balozi Mdogo wa China Zanzibar,Balozi Xie Xiuowu, akimsikiliza Mgeni Rasmin Mhe Mohammed Aboud Mohammed akihutubia wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Karume Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Baadhi ya Wageni waalikwa katika hafla ya kumkaribisha Balozi Mdogo wa China Zanzibar Balozi Xie Xiuowu. Wakimsikiliza mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed.

Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi zao Zanzibar wakiwa katika hafla hiyo ya kumkaribisha Balozi Mdogo wa China ilioandaliwa na Ubalozi wa China Tanzania katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Madaktari wa Kichina waliopo Zanzibar wakihudhuria tafrija hiyo ya kumkaribisha Balozi Mdogo wa China.
Mgeni Rasmin katika Tafrija ya Chakula cha usiku kilichoandaliwa na Ubalozi wa China Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed akigonganisha glasi na Balozi Mdogo wa China Zanzibar Balozi. Xie Xiuowu kuonesha ishara ya ushirikiano wa Nchi hizi mbili wakati wa hafla hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.


Baadhi ya Wageni waalikwa katika hafla ya kumkaribisha Balozi Mdogo wa China Zanzibar Balozi Xie Xiuowu. Wakimsikiliza mgeni Rasmin Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed na Balozi Mdogo wa China Xie Xiuowu wakijumuika na wageni wengine wakijumuika katika chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao kumkaribisha Balozi huyo Zanzibar kuchukua nafasi iliochwa na balozi  aliyeondoka baada ya kumaliza muda wake wa kazi Zanzibar.
Viongozi wa Serikali na Wananchi walioalikwa katika hafla hiyo ya chakula cha usiku kumkaribisha Balozi Mdogo wa China Zanzibar wakipata chakula kilichoandaliwa na Ubalozi wa China Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi zao Zanzibar wakiwa katika hafla hiyo ya chakula cha usiku kumkaribisha Balozi Mdogo wa China Zanzibar wakipata chakula kilichoandaliwa na Ubalozi wa China Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. 
Viongozi wa Serikali na Wananchi walioalikwa katika hafla hiyo ya chakula cha usiku kumkaribisha Balozi Mdogo wa China Zanzibar wakipata chakula kilichoandaliwa na Ubalozi wa China Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. 


Baadhi ya Madaktari wa Kichina wanaofanya kazi katika hospitali ya Mnazi Mmoja wakipata chakula cha usiku kilichoandaliwa na Ubalozi wa Mdogo wa China Zanzibar kumkaribisha Balozi Mpya wa China Zanzibar,Xie Xiaowu, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.