Habari za Punde

Uzinduzi wa Mkutano wa Kongamano la Watanzania Wanaoishi Nje Diaspora Unaofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

Viongozi wa Serikali na Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Kongamano la Tatu la Watanzania Wanaoishi Nje Diaspora wakisubiri kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kumpokea kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano hilo katika Ukumbi wa Hateli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Karume akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza lac Mapinduzi Mhe Issa Haji Gavu alipowasili katika viwanja vya hoteli hiyo kuhudhuria Kongamano hilo.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud, wakielekea ukumbi wa mkutano.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo alipowasili katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort kwa ajili ya Ufunguzi wa Mkutano huo wa Kongamano la Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi Diaspora. 


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Afisa wa Mambo ya Nje wa Zanzibar akielekea kuangalia ngoma za utamaduni zilizoandaliwa kwa ajili ya Mkutano huo.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Maige wakielekea katika ukumbi wa Mkutano. 

Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiana ya Kimataifa na Diaspora Zanzibar Bi Adila akizungumza na Wanadiaspora na kuwakaribisha katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.