Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Yakabidhi Vifaa vya Ujenzi kwa Masjid Kauthar Nyamazi Unguja.

Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ) Imetumia zaidi ya shilingi Milioni Mia Mbili na Sabini kutoa mikopo ya Masomo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu katika kipindi cha mwaka huu. 
Akizungumza Afisa Masoko wa PBZ Ndg. Mohammed Nuhu wakati wa kukabidhi msaada wa vifaa vya Ujenzi mbalimbali kwa ajili ya Masjid Kauthar katika Kijiji cha Nyamazi Wilaya ya Magharibi B Unguja na kusema fedha hizo zimetolewa kwa Wanafunzi Mia Moja.

Amesama pamoja na Mikopo hiyo pia imetoa mkopo kwa Watu Ishirini na Sita ili kushiriki katika Ibada ya Hijja mwaka huu.
Afisa Masoko huyo wa PBZ Ndg. Mohammed Nuhu amesema utaratibu huo wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ni kutekeleza azma ya kuwa karibu na Jamii katika utoaji wa huduma zake pamoja na maendeleo yao katika kusaidia jamii mbalimbali Zanzibar.,
Imamu wa Masjid Kauthar Shekh. Khamis Jecha Pandu, ametowa shukrani kwa PBZ kutokana na masaada wao huo kukamilisha ujenzi wa Masjid yao katika Kijiji chao cha Nyamanzi na kuwataka Wananchi na Wafanyabiashara wa Zanzibar kujitokea kusaidia ujenzi wa Masjid hiyo ili kutoa fursa kwa Wananchi wa Nyamanzi kuutumia msikiti huo kwa Ibada. 

Shekh Jecha amesema Masjid yao inahitajika kiasi cha shilingi milioni 56, kukamilika kwa ujenzi huo. Na kutoa namba yake ya simu kwa Wananchi watakao hitaji kutoa mchango wao wanaweza kuwasiliana kwa No hii.0777850344. 
Jengo la Masjid Kauthar lilioko katika Kijiji cha Nyamanzi Unguja Wilaya ya Magharibi B likiendelea na Ujenzi wake linahitaji Msaada wako kuweza kumalizia ujenzi huo na kutoa huduma ya Ibada kwa Wananchi wa Kijiji hicho unaweza kuwasiliana na Msimamizi wa Msikiti huo Shekh Khamis Jecha Pandu kwa Namba hii 0777 850344. Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akikabidhi vifaa vya Ujenzi wa Masjid Kauthar akipokea msaada huo Sheikh Khamis Jecha Pandu PBZ imekabidhi vifaa vya ujenzi huo Jipsum, Saruji na Misumari ili kumalizia ujenzi wake huo.
Shekh Khamis Jecha Pandu akitowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ na Wafanyakazi wake kwa Msaada wao kuwezesha kualizia ujenzi wa masikti huo,  
Afisa Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Mohammed Nuhu akisalimiana na Shekh Khamis Jecha Pandu msimamizi wa ujenzi wa Masjid Kauthar Nyamanzi Unguja. wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kumalizia msikiti huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.