Habari za Punde

Zoezi la Uondoaji wa Makonteni Eneo la Darajani Likiendelea Baada ya Kuvunjwa Maskani ya Dk Bilal Mbele ya Skuli ya Vikokotoni.

 Enelo la Makonteni ya Maskani ya Bilal Darajani baada ya Wafanyabiashara wa eneo hilo kuvunja  maduka yao ili kupisha Ujenzi wa Maduka ya Kisasa katika eneo hilo la darajani.

Wananchi wa Mji wa Unguja wakiangalia kijiko cha Baraza la Manispa Zanzibar likisafisha katika eneo hilo baada ya wenye eneo hilo la biashara kuvunja juzi usiku ili kupisha Ujenzi wa Maduka ya Kisasa yanayotarajiwa kujengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuimarisha Mji Mkongwe wa Zanzibar. 

1 comment:

  1. Weshajipanga na fedha wanazo ? Maana miradi na mipango mingi ila pesa na ubunifu haupo !! Kama sio Bakhresa Ile barabara ya fuoni ndo ingekuwa imebaki ya vumbi tu !!! Tusikurupuke tu aidha kutokana na sababu za kisiasa au mipango isoyoyumkini Kwa mda huu.Kila la kheri

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.