Habari za Punde

Dk Shein Akutana na Balozi mpya wa Msumbiji nchini

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Bibi,Monica Patricio Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais leo,(katikati) Balozi Mdogo wa Msumbiji anyefanyia kazi zake Zanzibae Bw. Jorge Augusto Menezes,[Picha na Ikulu.]07/09/2016.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio  mara  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha leo,[Picha na Ikulu.]07/09/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Bibi,Monica Patricio (wa pili kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana nao mara  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]07/09/2016.


STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
  Zanzibar                                    7.08.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Msumbiji na Tanzania ni nchi zenye historia katika uhusiano na ushirikiano wao hivyo kuna haja ya kuendelezwa na kuimarishwa zaidi kwa manufaa ya pande mbili hizo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati wa mazungumzo kati yake na Balozi mpya  wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniam Monica Patricio Clemente Mussa  aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alisema kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbuji ni wa kihistoria ambao umeasisiwa na viongozi wa wa Mataifa hayo akiwemo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume na Hayati Samora Machel.

Akisisitiza juu ya uhusiano na ushirikiano wa kidugu kati ya Zanzibar na Masumbiji, Dk. Shein alisema kuwa katika kuliimarisha hilo Zanzibar hivi sasa kuna WanaMsumbujini wengi wanaoishi na waliozaliwa ambao wanaishi na Wazanzibari kama ndugu.

Kutokana na juhudi na hatua hizo, Dk. Shein alisema kuwa mashirikiano katika sekta kadhaa za maendeleo ni muhimu na ya msingi kwani yanaweza kuleta tija na mafanikio zaidi kwa pande zote.

Aidha, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa mafanikio makubwa iliyoyapata Msumbiji katika kuimarisha uchumi wake sambamba na mafanikio katika sekta nyengine za maendeleo.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini sana uhusiano na ushirikiano huo uliopo kati ya Msumbiji na Zanzibar na kueleza kuwa mashirikiano yanayoendelezwa yatasaidia katika uimarishwaji wa sekta za maendeleo zikiwemo elimu, kilimo, gesi na mafuta, biashara, utalii na nyenginezo.

Akizungumzia kwa upande wa sekta ya elimu, Dk. Shen alisema kuwa Zanzibar imeweza kupiga hatua katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwa na Vyuo Vikuu Vitatu hivi sasa na kusisitiza haja kwa Msumbiji kuleta wanafunzi wake ili kuja kusoma Zanzibar ikiwa ni pamoja na kujifunza Lugha ya Kiswahili kupitia Chuo chake Kikuu cha Taifa cha SUZA.

Pia, Dk. Shein akitilia mkazo sula hilo alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia katika kubadilishana uzoefu ambapo itawapa fursa na wanafunzi wa Zanzibar kwenda nchini humo kusoma lugha ya Kireno kwa lengo la kuiimarisha lugha hiyo hapa nchini ambayo ina historia kubwa katika historia ya Zanzibar na Utawala wa Kireno uliotawala hapa Zanzibar mnamo miaka ya 1500.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumkaribisha Balozi huyo hapa nchini pamoja na kumpongeza Rais wa Nchi hiyo  Filipe Nyusi kwa mafanikio yaliopatikana ya kiuchumi na kimaendeleo.

Nae Balozi wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Monica Patricio Clemente Mussa, alisema kuwa Msumbiji inajivunia uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ikiwemo Zanzibar ambao ni wa muda mrefu.

Katika maelezoa yake Balozi huyo wa Msumbiji alisema kuwa  nchi hiyo hivi sasa imeqweza kupata mafanikio makubwa kwani tayari uchumi wake unazidi kuimarika siku hadi siku.

Aidha, Balozi Mussa alisema kuwa miongoni mwa sekta ambazo hivi sasa zinaimarika ni pamoja na sekta ya miundombinu, kilimo, madini, gesi na mafuta huku akisisitiza kuwa uchumi wa nchi hiyo inaendelea kukua na kuimarika.

Katika mazungumzo yao viongozi hao pia, waligusia haja ya kukuza uhusiano na ushirikiano katika sekta za  maendeleo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.