Habari za Punde

Kampuni ya Nowe yamnyong’onyesha waziri wa fedha Pemba


 Na Haji Nassor, Pemba
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed, amesema haridhishwi hata kidogo na kusuasua ya ujenzi wa jengo jipya la baraza la mji Chakechake Pemba, linalojengwa na kampuni ya Nowe Investment Co LTD ya Tanzania bara.
Alisema ukarabati na ujenzi unaofanyika kwa ofisi ya baraza la mji Mkoani unaridhishwa, ingawa kwa ujenzi wa jengo hilo la Chakechake hali imekuwa sio ya kuridhisha na kumtaka mjenzi kuhakikisha anakuwa makini kwenye kazi zake.
Waziri huyo alitoa tamko hilo jana wakati alipokuwa akizungumza na mhandisi mjenzi wa kampuni hiyo,  kwenye jengo hilo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku tatu kisiwani Pemba ya kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Alisema alitarajia sana kampuni za kizalendo zionyeshe umahiri na ukakamavu wanapopewa kazi, ingawa kwa kampuni ya Nowe Investment, kazi yao kwenye jengo hilo hairidhishi.
Aidha Waziri huyo wa fedha alimueleza mjezni huyo kuwa lazima sasa waongeze idadi wa watendaji kazi (vibarua) na kuhakikisha wanaongeza muda wa kazi, ili jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati mwafaka.
Alifafanua kuwa kama kipindi cha mkataba wa awali kimeshapita bila ya kulikamilisha, lazima sasa waheshimu na wathamini miezi mitano waliopewa, katika ujenzi wa jengo hilo.
Aidha aliongeza kuwa, sio busara kwa kampuni zenye makao makuu yake Tanzania bara, wakubwa kujifungia huko na kuwaacha vibarua wakiendesha ujenzi.
“Sasa kama mmeomba miezi mitano mengine sawa, lakini na nyinyi acheni kujifungia Tanzania bara, kuweni kwenye kazi zenu muda wote, ili mkamilishe kazi kwa wakati’’,alifafanua.
Mapema Mhandisi wa jengo hilo kutoka kampuni hiyo Elmeka A. Shuma, alisema kulikuwa na mambo kadhaa yaliosababisha kutokamilisha ujenzi huo kwa wakati, ikiwemo kuchelewa kupewa uamuzi baada ya kuomba jambo.
“Muheshimwa waziri tukikaa miezi zaidi ya mitatu, twangoja tujibiwe kama tuvunje ujenzi wa awali au laa, lakini hata uwekaji wa jamvi kupewa jawabu nako kulichelewa”,alifafanua.
Kwa upande mkandarasi wa jengo hilo na  ukarabati wa jengo la baraza la mji Mkoani, Joseph Maradu kutoka kampuni ya Mekon Consultant Engineering, alimueleza Waziri huyo kuwa kutokuwa makini kwa baadhi ya kampuni za kizalendo ndio tatizo.
“Mimi naona kuchelewa kwa jengo hili la ofisi ya baraza la mji Chakechake, kwa baadhi ya kampuni za kizalendo kutokuwa makini na kazi zao na kujisahau’’,alifafanua.

Awali Waziri huyo wa fedha na ujumbe wake, ulitembelea pia ujenzi wa barabara ya Ole –Kengeja yenye urefu wa kilomita 35 barabara ya Mgagadu –Kiwani yenye uref wa kilomita 6.3, zoezi la ununuzi wa karafuu kituo cha Mkoani na Hospitali ya Abdalla mzee Mkoa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.