Alex
Kamamia wa Ericsson (wa pili kulia)
akielezea jinsi mtambo mpya wa mawasiliano ya Zantel utakavyoboresha huduma kwa
watumiaji wa mtandao wa Zantel. Wakimsikiliza ni Mkuu wa Ufundi wa Zantel Larry
Arthur (kushoto) na Jx Chen wa Huawei (wa pili kushoto) na Frode Dyrdal (kulia)
wa Ericsson.
Meneja
Miradi wa Zantel Zanzibar Mohamed Ahmed Jaye, akielezea waandishi wa habari
(hawapo pichani), jinsi mitambo mipya ya Zantel inavyofanya kazi. Zantel
imeanza mradi mkubwa wa kuborersha mtandao wake nchi nzima kwa kufunga mitambo
mipya ya mawasiliano kwa ushirikiano na Huawei Technologies na Ericsson.
Mkuu
wa Ufundi wa Zantel Larry Arthur (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu uboreshwaji wa mtandao wa Zantel baada ya
kuwasili vifaa vipya kutoka Ericsson na Huawei Technologies. Kushoto ni William
Cheng (Wei) kutoka Huawei, wa pili kushoto ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed
Khamis Mussa(Baucha), na kulia ni Frode Dyrdal wa Ericsson
Mkuu
wa Zantel Zanzibar Mohamed Khamis Mussa-Baucha (Kulia) akisisitiza jambo wakati
wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uboreshwaji wa mtandao wa Zantel baada ya
kuwasili vifaa vipya kutoka Ericsson na Huawei Technologies. Akimsikiliza ni
afisa wa Huawei William Cheng (Wei)
Mkuu
wa Zantel Zanzibar Mohamed Khamis Mussa (kulia) akifurahia jambo na maafisa
waandamizi kutoka Zantel, Ericsson na Huawei, baada ya mkutano na waandishi wa
habari kuelezea mtandao ulioboreshwa wa Zantel unaoanza kujengwa hivi karibuni.
Mradi wa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu.
Mkuu
wa Zantel Zanzibar Mohamed Khamis Mussa (wa pili kulia) na Mkuu wa Ufundi wa
Zantel Larry Arthur (wa pili kushoto), wakipongezana na wadau wao wakubwa
katika uboreshaji wa mtandao za Zantel unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi
mitatu ijayo. Kulia ni Frode Dyrdal wa Ericsson na kushoto ni William Cheng wa
Huawei.
Baadhi
ya vifaa vipya vilivyowasili Zanzibar kutoka kampuni za Ericsson na Huawei
Technologies tayari kwa uboreshaji wa mtandao wa Zantel katika mradi wenye
gharama ya zaidi ya Tsh. 2bn/- unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu.
Baada ya kukamilika watuamiaji watapata mawasiliano yenye ubora zaidi.
Maafisa
waandamizi wa Zantel, Huawei Technologies na Eriscsson, wakiongea na waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu uboreshaji wa mtandao wa Zantel katika
mradi wenye gharama ya zaidi ya Tsh. 2bn/- unaotarajiwa kukamilika ndani ya
miezi mitatu.
Picha zote na Martin Kabemba
No comments:
Post a Comment