WASHIRIKI wa mkutano wa kuongeza Tathmini za athari
za mazingira Zanzibar, wakimsikiliza kwa makini mgeni Rasmi katika Mkutano huo
wakati alipokuwa akifungua mkutano huo uliofanyika nje ya mji wa Chake Chake
Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MTAALAMU kutoka Kamisheni ya Tathmini za Kimazingira
nchini Netherlands, Ineke Steinhauer akiwasilisha mada katika mkutano huo wa
Tathmini ya athari za Mazingira Zanzibar uliowashirikisha wadau kutoka taasisi
mbali mbali za Serikali na Binafsi zinazojihusisha na masuala ya mazingira.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira
Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akiwasilisha mada ya matokeo ya Tathmini za athari
za Mazingira kwa wadau wanaohusika na masuala ya kimazingira Kisiwani Pemba,
mkutano huo uliofanyika nje ya mji wa Chake Chake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWAKILISHI wa Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na
Usafirishaji Pemba, Ali Mohamed akichangia katika mkutano huo wa tathmini za
kimazingira.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na
Mazingira Juma Bakari Alawi, akifungu mkutano wa matokeo ya Tathmini za athari
za Maizngira kwa wadau kutoka taasisi mbali Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
AFISA Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na
Mazingira Juma Bakari Alawi, akijadiliana jambo na Mtaalamu kutoka Kamisheni ya
Tathmini za Kimazingira nchini Netherlands, Ineke Steinhauer mara baada ya
kufunga kwa mkutano wa kutathmini athari za matokeo ya Mazingira Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
AFISA Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na
Mazingira Juma Bakari Alawi, akijadiliana jambo wataalamu mbali mbali juu ya mkutano
wa kutathmini athari za Mazingira Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MWEZESHAJI wa mafunzo ya matokeo ya Tathmini za
athari za Mazingira Dk Aboud S Jumbe, akiwasilisha mada katika mkutano huo
uliowakutanisha wadau kutoka taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi
zinazojihusisha na masuala ya Mazingira.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment