Habari za Punde

Ufadhili wa masomo ya uzamivu katika fani ya Elimu ( PHD in Education)

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR TANGAZO LA UFADHILI WA MASOMO YA UZAMIVU KATIKA FANI YA ELIMU (PHD IN EDUCATION)

 CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA) KUPITIA MRADI WAKE WA TRANSLED UNAOFADHILIWA NA SHIRIKA LA NORAD KINATANGAZA UFADHILI WA MASOMO YA UZAMIVU KATIKA FANI YA ELIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM. 

MUOMBAJI ATAKAECHAGULIWA KUENDELEA NA MASOMO YA CHUO NA KUKUBALIWA NA SUZA KUTOKANA NA MAHITAJI ILIYONAYO, MASHARTI YA MKATABA ATAKAOFUNGA NA SUZA NA MASHARTI YA MRADIATAPATIWA UFADHILI WA MASOMO IKIWEMO ADA YA MASOMO (TUITION FEES), MALIPO YA MOJA KWA MOJA (DIRECT COSTS) NA UTAFITI (RESEARCH) KWA MIAKA YOTE YA MASOMO. 

MUOMBAJI ANATAKIWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO

1. KUJAZA FOMU YA MAOMBI YA ONLINE ILIYOPO KWENYE TOVUTI YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM AMBAYO NI http://postgraduate.udsm.ac.tz/

 2. ATATAKIWA KUCHAGUA PhD IN EDUCATION BY COURSEWORK NA DISSERTATION. KATIKA SEHEMU YA BARUA YA MWAJIRI SI LAZIMA KUAMBATANISHA ANDIKA TU “NINAYO”, NA PIA BARUA YA SPONSOR ANDIKA “TRANSLED PROJECT FUNDED BY NORAD”.

 3. ATATAKIWA KUTUMA MAOMBI YA UFADHILI AKIAMBATANISHA CHETI CHA KUZALIWA, VYETI VYOTE VYA MASOMO, NA SABABU NA USHAHIDI WA YEYE KUPATIWA UFADHILI WA MASOMO NA BARUA YA KUKUBALIWA NA CHUO (ADMISSION LETTER). BARUA YA MAOMBI YA UFADHILI IANDIKWE KWA KIINGEREZA NA IPELEKWE KWA MRATIBU MKUU WA MRADI WA TRANSLED.CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR, P. O. BOX 146, ZANZIBAR. 

MUOMBAJI ATAKAE FADHILIWA NA MRADI ANATAKIWA KUWA NA SIFA ZIFUATAZO: 

1. AWE MZANZIBARI 
2. AWE NA DIGRII YA UZAMILI KATIKA FANI YA ELIMU AU NYENGINEYO INAYOSHABIHIANA. 
3. IWAPO HANA DIGRII YA UZAMILI YA FANI YA ELIMU AU INAYOSHABIHIANA BASI AWE NA DIGRII YA UZAMILI NYENGINE LAKINI AWE ANAYO SHAHADA YA KWANZA YA FANI YA ELIMU NA SAYANSI (BSC. WITH EDUCATION) AU ELIMU NA SANAA (B.A. WITH EDUCATION). 

WAOMBAJI WATAKAOPEWA KIPAUMBELE: 

1. PAMOJA NA SIFA ZILIZOTAJWA WAOMBAJI WATAKAOPEWA KIPAUMBELE NI WALE WASIO NA UWEZO WA KUJISOMESHA, MAYATIMA, WANAWAKE, WATU WENYE ULEMAVU, WATU WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU. 

2. WALIOSOMA SHAHADA YA KWANZA AU YA PILI (UZAMILI) KATIKA FANI YA SAYANSI NA ELIMU (SCIENCE WITH EDUCATION) AMBAO WALICHUKUA MASOMO YA BIOLOJIA, KEMIA, FIZIKIA NA HESABU. WALIOSOMEA SANAA NA ELIMU KATIKA MASOMO YA JIOGRAFIA NA HISTORIA WANAWEZA KUFADHILIWA IKIBIDI. 

3. WALIOSOMA FANI YA ELIMU MJUMUISHO (INCLUSIVE EDUCATION), FANI YA ELIMU AWALI AU AU ELIMU KWA MICHEZO NA SAYANSI YA MICHEZO, AIDHA KATIKA SHAHADA YA KWANZA AU YA PILI. 

ZINGATIA 

WATAKAOLETA MAOMBI YA UFADHILI NA VIELELEZO VYOTE IKIWEMO BARUA ZA KUKUBALIWA NA CHUO (ADMISSION LETTER) KWA MRATIBU WA MRADI WA TRANSLED MWANZO NA WENYE SIFA ZILIZOTAJWA NDIO WATAKAOPATA UFADHILI (FIRST COME FIRST SERVED). WATAKAOFADHILIWA NI WAOMBAJI WATATU TU. 

MWISHO WA KUWASILISHA MAOMBI NI ALHAMISI TAREHE 29 SEPTEMBA, 2016. KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA 0778000313 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.