Habari za Punde

Mkutano wa kuhamasisha udhibiti wa Zao la Karafuu

Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Zanzibar Mhe. Juma Ali Khatib akizungumza na Masheha wa Wilaya ya Chakechake Pemba, wakati wa mkutano huo wa kuhamasisha udhibiti wa Zao la Karafuu Kisiwani huo, wakati wa msimu huu wa zao hilo kutotoa fursa kwa Wahujumu wa Uchumi wa Karafuu Pemba kutopata fursa ya kusafirisha zao hilo kwa magendo. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Mhe Said Soud Said akizungumza na Masheha wa Wilaya Chakechake Pemba kuzungumzia kudhibiti zao la Karafuu Kisiwani Pemba kulia Mhe Juma Ali Khatib.wakiwa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba, Mkutano huo umewajumuisha Masheha wa Wilaya ya Chakechake Pemba.
Baadhi ya Masheha wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, wakiwasikiliza Mawaziri wasiokuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Said Soud Said na Juma Ali Khatib , huko katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa Kusini Pemba, juu udhibiti wa magendo ya Karafuu(Picha na Bakar Mussa -Pemba).
Sheha wa Shehia ya Mkoroshoni Pemba, Khamis Idd Songoro, akichangia neno katika mkutano wa Masheha na Mwaziri wasiokuwa na Wizara maalumu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, huko katika ukumbi  wa Ofisi ya

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.