Habari za Punde

Balozi Seif akutana na uongozi wa kampuni ya kimataifa ya uwekezaji vitega uchumi ya Koyo nchini Japan

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Nchini Japan  Bwana Norio Shoji Nyumbani kwake Bara bara ya Haile Selassie Jijijini Dar es salaam.
 Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyokutoka Japan  ukiongozwa na Rais wa  Kampuni ya  Kimataifa ya Uwekezaji ya  Koyo kutoka Nchini Japan  Bwana Norio Shoji wa Pili kutoka Kulia ukibadilishana mawazo na Balozi Seif.
 Bwana Norio Shoji akimueleza Balozi Seif shauku ya Kampuni yake kutaka kuwekeza vitega Uchumi Nchini Tanzania kulingana na mazingira na rasilmali zilizopo.

Balozi Seif akibadilishana mawazo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya  Koyo kutoka Nchini Japan  Bwana Norio aliyepo kati kati mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika nyumbani kwake Bara bara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam.


Wa kwanza kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa  Kampuni ya Kimataifa yaUwekezaji ya  Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Koichi Kawaji.

Picha na – OMPR – ZNZ.

NA Othman Khamis, OMPR

Kasi kubwa ya uchumi wa Tanzania inayoonekana kupanda kwa haraka katika kipindi kifupi imeanza kutoa ushawishi mkubwa kwa Makampuni na Taasisi za Kimataifa kuonyesha dalili za  kutaka kuwekeza miradi yaoya Kiuchumi na maendeleo ili kuunga mkono kasi hiyo.

Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo kutoka Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi Kawaji akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Sita wa Kampuni hiyo  alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Bara ara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam.

Bwana Koichi Kawaji alisema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na Wataalamu wa masuala ya Uchumi Duniani  umebaini kwamba  kasi ya uchumi wa Taifa la Tanzania unaongoza ikilinganishwa na Mataifa
yaliyomo ndani ya Bara la Afrika kwa hivi sasa .

Kiongozi huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Koto  alifahamisha kwamba Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika yenye muelekeo mpana wa Uchumi wake kukuwa kwa haraka ukifananishwa na Nchi ya Singapore Bwana  Koichi alisema wataalamu wa Kampuni ya Koyo wamelazimika kufanya ziara ya makusudi katika azma ya kujionea kasi hiyo Nchini Tanzania na kuangalia maeneo ambayo Taasisi hiyo ya Uwekezaji inaweza kutumia fursa zilizopo katika kusaidia ukuaji wa Uchumi wa Tanzania.

Alieleza kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilmali za kutosha za Kiuchumi ambazo kwa namna nyingi Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchini wanaweza kutumiwa vyema katika njia ya kuingia ubia na Serikali,Makampuni au hata Watu binafsi wenye sifa na shauku ya kuwekeza.

Rais huyo wa Kamuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo kutoka Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi alielezea furaha yake kutokana na utulivu mkubwa na Amani iliyotanda Nchini Tanzania katika kipindi kirefu sasa.

Alisema amani na utulivu huo kwa kiasi kikubwa ndio iliyozaa mafanikio makubwa ya Uchumi yanayoendelea kupatikana na hatimae kuchangia mapato ya Taifa  sambamba na kupunguza umasikini  lakini kwa njia nyengine pia umezuia mfumko wa bei unaotoa afueni ya maisha bora kwa Wananchi walio wengi.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishauri Serikali ya Japani kupitia ujumbe wa Kampuni hiyo ya Koyo kuangalia maeneo ambayo Taasisi na Makamuni ya Nchi hiyo yanawekakuwekeza.

Balozi Seif alisema Tanzania imepakana na Bahari kuu eneo ambalo Japan kutokana na kuendelea Kiviwanda inaweza kusaidia Taa luma katika Mpango wa kulielekeza Taifa la Tanzania kuwa Nchi ya  Viwanda ifikapo Mwaka 2025.

Alisema Tanzania bado ina fursa nzuri ya kujifunza Taaluma ya Uvuvi wa Bahari kuu kwa kuanzishwa Viwanda vya usindikaji  bidhaa zinazotoka na mazao ya Baharini kama Samaki wa aina mbali mbali pamoja na zao la Mwani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni hiyo ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibat itakuwa tayari kutoa msaada wowote utakaohitajiwa na Kampuni hiyo wakati itakapofikia hatua ya kutaka kuwekeza  miradi yake Visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.