Habari za Punde

Ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Siasa Uhusiano wa Kimataifa Mhe Hamad Yussuf Masauni Kutembelea Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Wananchi wa Zanzibar.

Katibu wa Kamati ya Maalum NEC Idara ya Siasa Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng. Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya ya Mjini kabla ya kuaza kwa ziara yake kuangalia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. kwa Miradi ya Jamii katika Wilaya hiyo.    
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Uhusiano wa Kimataifa Mhev Eng Hamad Yussuf Masauni akitembelea ujenzi wa barabara ya gofu gymkhana ikiwa ni moja ua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Wananchi wa Zanzibar akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja akiwa na Viongozi wa CCM Mjini.
Sheha wa Shehia ya Kikwajuni Ndg Juma Saadat akitowa maelezo kwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Eng. Hamad Yussuf Masauni akimsikiliza Shehia huyo akitowa maelezo kuhusu athari waliopata wananchi swa shehia yake wakati wa ujenzi wa barabara ya ndani kutoka klabu ya kikwajuni hadi bosnia nyumba hizo zimepata mtikisiko. 
Sheha wa Shehia ya Kikwajuni Ndg Juma Saadat akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni eneo la athari iliotokea wakati wa ujenzi huo wa barabara. ikiwa ni kuimarisha miundombinu ya barabara za ndani katika maeneo ya Unguja.
Katibu wa Tawi la CCM Muembeladu Jimbo la Kikwajuni Ndg Juma Sumbu akitowa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Tawi hilo kwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni wakati wa ziara yake kuona maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Wananchi wa Zanzibar. 
Katibu wa CCM WEilaya ya Mjini Bi Fatma Shomari akizungumza wakati wa ziara hiyo wakiwa katika ukumbi wa Tawi la CCM Muembeladu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Bi Fatma Shomar akizungumza na wananchi wa Tawi la CCM Muembeladu kabla ya kumkaribisha Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Mhe. Hamad Yussuf Masauni akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Mjini Unguja.  





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.