JAMII
bado inauelewa mdogo kuhusu taka, sio wengi wenye uelewa kama taka ni muhimu na
zina faida kubwa kwa maisha ya kila siku.
Badala
yake huchukuliwa kama ni uchafu wenye kukirihisha kiasi ya kutothaminiwa na
kutunzwa kwenye mazingira mazuri kwa kuamini kutokua na matumizi wala faida
kwao.
Wanamazingira
wanaamini hakuna kisichofaida kinachotokana na taka taka ziwe za majumbani,
maskulini hata viwandani, ikiwa zitajengewa mazingira yakutumika tena la kuleta
faida kwa jamii na uchumi.
Jamii
inatambua suluhisho pekee la taka ni kuchomwa moto na kuangamizwa, suala ambalo
linapingwa na wanamazingira, ambao wanaeleza moshi unaotokana na takataka ni
sumu kwa afya za binaadamu na viumbe anuai (bio diversity).
Mradi
wa Ikolojia katika skuli za ukanda wa bahari ya Hindi maarufu kama "Eco
Schools" unaratibiwa na Kamisheni ya Bahari ya Hindi (IOC) chini ya
ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU).
Ulianzishwa
kwa awamu ya kwanza mwaka 2011 ambao unatekelezwa na skuli 45,000 kutoka nchi
sita za visiwa duniani, zikiwemo Re- Union, Visiwa vya Comoro, Madagascar,
Maurituis, Syschelles na Zanzibar kwa Tanzania.
Zanzibar
mradi uliletwa na Wizara ya Ardhi Maji Nishari na Mazingira nakuratibiwa na Jumuiya ya Mandeleo ya Vijana, Elimu na Mazingira, Zanzibar (ZAYEDESA) chini
ya utekelezaji wa kamati ya kitaifa ya ZNSC iliyozishirikisha taasisi
mbalimbali za umma na binafsi kwa ushirikiano na Wiraza ya Elimu na Mafunzo ya
Amali, Zanzibar.
Itakumbukwa
kuwa mwezi Oktoba mwaka jana, Mwenyekiti wa ZAYEDESA Mama Shadya Karume alizindua rasmi mradi wa "Eco-
schoosl" kwa Zanzibar, pale skuli ya "Stone Town Internation"
Migombani mjini Unguja.
Katika
uzinduzi wake, Mama Shadya alisisitiza suala la utunzaji mazingira endelevu kwamba
hujengwa na jamii hasa vijana ambao aliwaelezea kama ni nguvu kazi ya udhibiti
wa mazingira, ili yasiharibike kwani vijana ni wadau wakubwa.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu mradi wa Ikolojia (Eco Schools) kupelekwa mashuleni kupitia Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mama Shadya alisema anaamini elimu ina uwezo
mkubwa wa kufanya mabadiliko. Sambamba nakueleza kuwa elimu ndio chanzo cha
maendeleo endelevu.
Mama Shadya ambae pia ni mke wa
rais wa Zanzibar mstaafu awamu ya tano, Mhe. Amani Abeid Karume
anawaelezea vijana na watoto kwamba wanahitaji kupatiwa elimu ya kutosha kuhusu
athari za uchafuzi wa mazingira.
Kamati
ya taifa ZNESC imeteua skuli 30 za uma na binafsi kwa msingi na sekondari kwa
Unguja na Pemba ambapo Unguja skuli 20 zikiwemo 13 za umma na saba binafsi
wakati Pemba skuli 10, nane za umma na mbili binasi kwajili ya majaribio ya
mradi wa "Eco Schools"
L: Sifa za skuli kujiunga kwenye
programu ya "Eco Schools"
Ili
skuli iingie kwenye mchakato wa ikolojia, nilazima ifuate muuongozo uliotolewa
na Kamisheni ya Bahari ya Hindi (IOC) ambao unalazimisha skuli kutekeleza njia
saba muhimu za "Eco" ikiwemo kujisajili kwenye tovuti ya kimataifa ya
"Eco Schools" ambayo inaunganisha skuli zote zinazotekeleza mradi huo
duniani, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu na kujuana.
Aidha
skuli hulazimika kuwa na miongoni mwa shughuli zinazotekelezwa na programu ya
Eco ikiwemo miradi ya taka, umeme, maji, afya, viumbe hai, miradi inayohusisha
bahari na fukwe zake, miti asilia, bustani, misitu, upepo, matumbawe na mabadiliko
ya hali ya hewa kwa kuanza na walo mitatu na kuitekeleza.
Miradi
hiyo kwa lugha ya "Eco" hujuulikana kama "Eco theme"
sambamba na skuli kulazimika kuunda kamati ya ikolojia itakazishirikisha jamii
iliyoizunguka mazingira ya skuli husika wakiwemo majirani, walimu na wanafunzi
na viongozi wa shehia zao.
Kwamujibu
wa mwongozo huo wa kimataifa, Kamati ya "Eco" ni lazima iongozwe na
wanafunzi wenyewe pamoja na kuweka kumbukumbu kwenye jalada maalum kutokana na shughuli zote za Eco zinazofanyika
maskulini.
"School
code" ni sawa na sera ama sheria mama ambayo skuli teule katika programu
ya "Eco Schools" italazimika kuianzisha ambayo itabeba dhima nzima ya
"Eco" kutokana na jina la skuli husika.
Hata
hivyo mwongozo unalazimisha "code" za skuli ambazo zitaelezea
vipaumbele vya kimazingira ambavyo skuli inavitekeleza kwenye program hiyo. Mathali
skuli ya "Kwetu Bilingual" iliyoko Nungwi, Wilaya ya Kaskazini
"A" Unguja imetoka na code ya (Shajihisha mazingira, kwa kulinda
dunia).
Mwongozo
wa kimataifa wa programu ya ikolojia maskulini unalazimisha "Code"
hiyo kutambulikana kwenye mazingira ya ndani na nje ya skuli zote teuli za
Unguja na Pemba, si kwa wanafuzi pekee na walimu hata wanajamii walio karibu na
skuli hulazimika kuijua.
Mbali
na mafanikio machache yaliyofikiwa na programu ya "Eco schools" kwa
kufanikiwa kupatikana kwa skuli tatu tuu za Unguja kati ya 30 teule kwa Unguja
na Pemba.
Maalim Hamza Rijaal ambae ni
mjumbe wa kamati ya ZNESC kutoka Jumuiya ya Mazingira ya CODECOZ, anaeleza skuli
zilizofuzu kwenye program ya "Eco" ni Ben Bella kwa skuli za umma na
mbili binafsi zikiwemo "Stone Town Internation School" kwa wilaya ya
mjini Magharibi, Unguja na Mahaad Istiqama iliyoko wilaya ya kati, mkoa wa
Kusini Unguja.
Aidha
alieleza skuli ya "Kwetu Bilingual" iliyoko Nungwi na ile ya umma ya
Umoja sekondari huko Wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja pamoja na ya
"Connecting Continent" huko wilaya ya Wete Mkoa wa kusini Pemba
zinashika nafasi ya pili kwa kwenye kuiwakilisja "Eco".
L: Changamoto zinazo ukabili mradi
wa "Eco Schools," Zanzibar
Mwenyekiti
wa kamati ya taifa ya programu ya "Eco Schools" kwa Zanzibar, ZNESC ambae pia ni Ofisa ufuatiliaji na tathmini sekondari kutoka Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar, Maalim Khamis salum Khamis anaeleza
changamoto zinazozikabili skuli za umma katika utekelezaji
wa mradi huo.
Anasema kumekuwa na changamoto
nyingi kutokana na mradi kupokelewa na walimu wachache wanaousimamia kwa skuli
zote za umma na binafsi sambamba na kueleza ikitokea mwalimu kuhamishwa kituo
cha kufundishia ama kustaafu, skuli haibebi dhima ya kuusimamia na kuuedeleza
mradi huo.
Anasema
ikitokea kuwekwa mwalimu mwengine wa kusimamia programu hiyo kwenye skuli, huwa
haelewi chochote ndio maana mradi huzorota maskulini.
Mwl. Hamza Rijaal anaeleza uelewa
mpana zaidi bado unahitajika maskulini kutokana na kupatikana skuli chache zilizofanya
vizuri.
Alisema skuli za umma zimetoa ushiriki mdogo kwa kupatikana skuli
moja ambayo ni Ben bella kati ya 20 zilizoteuliwa na mradi ambapo binafsi
alieleza kupatikana skuli mbili za "Stone Town International na Mahaad
Istiqama"
Mkurugenzi
kutoka skuli binafsi ya "Stone Town International" ambae pia ni mjumbe
wa ZNESC, Bi. Jamila Jafar ambae anaeleza walivyofanikiwa kuzitathmini skuli za
unguja zinasotekeleza mradi wa "Eco"
"Tumegundua baadhi ya changamoto maskulini lakini tumewashauri na kuwapa
maelekezo jinsi ya kukabiliana na program hii, bila kutumia gharama ya fedha,
pia tumewashauri wawe wanabadilisha taaluma na uzoefu kupitia skuli zilizofanya
vizuri katika kufikia malengo yaliyokusudiwa". alieleza Bi. Jamila.
Mbali
ya changamoto zilizoonekana na kamati ya ZNESC, walimu kwa skuli zote za umma
na binafsi wanaeleza kuwa ushirikiano mdogo wanaoupata kwenye skuli
wanazozifundishia huchangia kurudisha nyuma juhudi za "Eco" pamoja na
morali ya walimu kufikia malengo ya mradi ikiangaliwa kuwa ni wa kujitolea
zaidi kuliko maslahi.
Mwalimu
Adam Shaaban Khatib kutoka skuli ya Umoja sekondari anaeleza kuwa hajawahi
kupata usaidizi kutoka kwa mwalimu yeyote katika skuli yake.
Awali
ZAYEDESA ilitoa mafunzo kwa walimu 21 wa skuli za majaribio ili kuendana
sambamba na mradi wa "Eco Schools" mapema mwezi Julai mwaka huu.
Tatizo
la lugha pia limetajwa kuwa kikwazo cha kupiga hatua mbele mradi wa "Ikolojia"
maskulini, hali iliyotajwa kurejesha nyuma juhudi za programu hiyo ambayo tageti
yake kubwa imeelekezwa kwa wanafunzi wa msingi na sekondari.
Maalim
Rijaali anaeleza kuwa mradi umefanikiwa zaidi kwenye skuli binafsi kutokana na
kuzungumzwa zaidi lugha ya kiiengereza ikilinganishwa na skuli za umma ambazo
mara nyinngi huzungumza lugha mama ya kiswahili.
Aidha
Walimu wanaosimamia mradi huo maskuli wameiomba kamati ya taifa, ZNESC kufanya
uwezekano wa kuwapatia muongozo wa kiswahili "Eco manual" kutokana na
jamii kubwa kuzungumza lugha ya kiswahili.
L:Mafanikio ya mradi maskuli /
kwenye jamii
Mradi
umeleta uweledi kwa wanafunzi kujifunza utunzaji mazingira endelevu kwa
vitendo.
Mwanafunzi
Habil Hilal wa kidato cha pili kutoka skuli ya Mahaad Istiqama anaeleza
alivyojifunza jinsi ya kuzibagua takataka
na manufaa yake ambapo alieleza kwenye skuli yao, wameweka sehemu nne
tofauti za kuhifadhia taka.
Anaeleza
wamefanikiwa kuzibagua taka ngumu kama vigae, mabati mabovu, karatasi, chupa na
majani kwa kila taka kuwekwa sehemu yake.
Sambamba
na kuzielezea taka zinazoweza kutumika kwa matumizi mbadala hufanywa hivyo.
"Tunazitumia
taka za majani kwa kufanya decomposition, pia tunatumia taka za majani kwaajili
ya mbolea ya bustani ya skuli yetu"
Anaeleza
mti ulioekewa taka za majani makavu unapata ubora kwa kuhifadhi maji kwenye miti hasa wakati wa kiangazi ambapo
jua hua kali na kuathiri mimea wakati wa joto kali.
Nae
mwanafusi Aisha Ali anaeleza taka za maji zinapozungushwa kwenye mmea husaidia
kuweka kivuli kwenye mmea, pamoja na kuondeza rutuba na kulinda "bio
deversity" kwenye udongo.
Aidha
Mwalimu mkuu kutoka skuli ya msingi kwetu "Bilingual" anaeleza
mafaniniko yao ya kuzigawanya taka kama walivyofanya Mahaad Istiqaama, Ben
bella na Stone Town International na ile ya "Conecting continent iliyoko
wilaya ya Chake chake, mkoa wa kusini - Pemba.
Mwalimu
mkuu kutoka skuli yamsingi Kwetu Bilingual, Mwanahamis Suleiman anaeleza taka
za chupa na plastiki huziuza kwa kampuni ya .....na fedha zinazopatikana huziingiza
kwenye mfuko wa skuli kwa maendeleo ya skuli hiyo.
Nae
mwalimu mkuu wa skuli ya "Stone Town International", Ingrid Verhulst anasema
wanafunzi skulini hapo hutumia karatasi kwa kuzifanyia mkaa ambao hutumika kwa
matumizi ya skuli kama kupikia.
Alielezea
"theme" nne zinazofanywa na wanafuzi wa skuli hiyo kwa mujibu wa
mwongozo wa program hiyo ya ikoloji ya mashuleni.
Alisema
skuli inafanya programu ya taka, fukwe za bahari ambapo kila Ijumaa huenda
ufukweni kuokota taka taka, programu ya nishati kwa kuwashajihisha wanafunzi
juu ya matumizi sahihi ya vifaa vya umeme wakiwepo skuli na hata majumbani mwao
kwa kuwakataza kutokutia taa wakati wa mchana ama feni sehemu isiyo watu.
"Wanafunzi
pia wanaimarisha kilimo cha mchaichai ambacho kimesanifiwa kama bustani inayopendeza
machoni pia hutumiwa kwa chai ya wanafunzi na wageni wanaofika skuli hapo"
alieleza.
Alisema
pia wanatumia boksi zilizotumika ambazo huzisanifu kwenye mwonekano mzuri na kuziweka kila darasa ambako wanafunzi huhufadhia
taka taka hasa za makaratasi.
"Tunamshirikisha
jirani yetu hapa muuza madafu kama sehemu ya mazingira yetu, tunatumia mafuu ya
madafu, tunayasanifu kwenye mwonekano mzuri kwaajili ya urembo wa mazingira ya
skuli yetu" alifahamisha Mwl. Verhulst
Aidha
anaeleza kuwa pia huzisanifu cd mbovu, kwa kutengeneza vibakuli vya kuhifadhia
vifaa vidogo vya skuli kama peni, raba na penseli za wanafunzi madarasani.
Skuli
ya "Stone Town International", ni moja kati ya skuli zinazohifadhi mbao
chakavu zinazotokana na thamani za skuli.
Programu
ya "Eco Schools" mbali na kutumiwa kwa mualama wa mazingira maskulini,
pia inaweza kutumika kama mitaala ya masomo ya kawaida yakiwemo ya masomo maskuli.
Mathalani
kupitia masomo ya lugha kama Kiingereza, kiswahili au kiarabu wanafunzi wataweza
kuandika insha, mashairi au uandishi wa barua zao kwa kuielezea "Eco".
"Eco
School" pia ina nafasi pana ya kuelezewa kwenye masmo ya jiografia, masomo
ya uraia, kupitia mada za mazingira kama ongezeko la idadi ya watu ama mada za
mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi wa mazingira.
Mwl. Hamza Rijaal, anaeleza hata
masomo ya sayansi kama fizikia biolojia, kemia
na hesabati yananafasi kubwa kwa wanafunzi kuielezea na kuifanya
"Eco" kiviitendo kupitia michoro ya "Pie chati na magrafi"
ambayo hutoa tafsiri nyepesi kwenye maelezo ya mada husika.
Skuli 30 teule za programu ya
ikolojia mashuleni kwa Zanzibar ni
pamoja na Ben Bella, Muungano msingi, Kijichi msingi, Kiembe samaki sekondari
na Mikindani kwa wilaya ya mjini Magharibi kwa skuli za umma.
Ambapo mkoa wa Kaskazini ni
pamoja na Potoa msingi, Mlimani sekondari, Donge msingi na Muanda sekondari.
Mkoa wa kusini Unguja, skuli ya
Dunga msingi, Mtende msingi, Umoja sekondari na Mtule sekondari.
Kusini Pemba Makombeni msingi,
Vitongoji msingi, Kangani sekondari na Fidel Castro sekondari.
Kaskazini Pemba, Chwaka - tumbe
sekondari, Makangali msingi na Wete sekondari.
Kwa upande wa skuli binafsi ni
pamoja na Stone town International, Lauriate Internatinal, Rainbow, Hifadhi na
Francis Maria kwa wilaya ya njini Magharibi.
Mahad Istikama pekee kwa mkoa
kusini Unguja, skluli za Kwetu Bilingual na Unique Learning kwa mkoa wa
Kaskazini.
Kwa upande wa Pemba ni skuli ya
Connecting Continet kwa Kusini na Ikra kwa mkoa wa Kaskazini.
ZNSC iliyozishirikisha taasisi za
umma na binafsi, wakiwemo Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira, Wizara ya
Elimu, Idara ya mazingira, Jumuiya ya skuli binafsi, Zanzibar (ZAPs).
Wengine ni Kisiwa cha Chumbe,
jumuiya ya Mazingira ya CODECOZ, Jumuiya ya wakulima wenye viwanda na masoko (ZNCCIA), mahoteli, wadau
wa elimu, vyombo vya habari.
mwashambajuma55@hotmail.com
+255
776 808 093
No comments:
Post a Comment