Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Cuba amaliza ziara ya kuitembelea Zanzibar

 Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa kushoto akioneshwa jambo na Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo kulia wakati akifanya matembezi katika mji Mkongwe wa Zanzibar,kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani.

Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa katikati akipita katika baadhi ya maeneo ya mji Mkongwe wa Zanzibar kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani
 Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa katikati akipata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo  Dk, Amina Ameri kulia wakati akitembelea maeneo ya mji Mkongwe wa Zanzibar kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Kushoto akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa wakikagua Gwaride rasmi katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kabla ya kuondoka leo na kurejea nyumbani.
Ndege iliompakia Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ikiacha aridhi na kuingia mawinguni baada ya kumaliza Ziara ya kikazi ya Siku moja Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.