Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein, Ajumuika na Mfalme wa Morocco katika Sala ya Ijumaa katika Masjid Mushawar Muembeshauri Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar,[Picha na Ikulu.]28/10/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa  ziara ya kibinafsi
Mfalme wa Morocco, Mohammed VI(kulia) akisalimiana na  Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga mara baada ya kuswalisha Swala ya Ijumaa katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa  ziara ya kibinafsi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa ziara ya kibinafsi Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali walihudhuria katika swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,na ujumbe wake waliswali kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakiwa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,na ujumbe wake waliswali kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 28/10/2016.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.