Habari za Punde

Mfalme wa Morcco Ajumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam Katika Sala ya Ijumaa Masjid Mushawar Muembeshauri Zanzibar.

Mfalme  Mohamed  VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed  Mahmoud alipowasili Msikiti wa Mushawara, Mwembeshauri, kutekeleza Ibada ya  sala ya Ijumaa katika Msikiti huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein akiwa na mgeni wake Mfalme Mohamed VI wa Morocco na baadhi ya viongozi wa Dini ya Kiislamu, wakiwa katika chumba maalum kilichojengwa ndani ya Msikiti wa Mushawar, Muembeshauri tayari kutekeleza ibada ya sala ya Ijumaa.
Mfalme Mohamed VI wa Morocco na ujumbe aliofuatana nao pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein wakisikiliza hotuba ya swala ya Ijumaa iliyotolewa na Imam na Khatib wa swala hiyo Sheikh Fadhil Suleiman Soraga.
Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na mgeni wake Mfalme Mohamed VI wa Morocco, wakiitikia dua baada ya ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Mushawar Muembe Shauri Zanzibar inayosomwa na Sheikh Fadhil Soraga.   
Mfalme Mohamed VI wa Morocco akimuonyesha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,Misahafu ambayo aliitowa zawadi kwa waumini katika Msikiti wa Mushawara, Mwembeshauri Mjini Zanzibar.
Mfalme Mohamed VI wa Morocco akimkabidhi Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi Masahafu baada ya kumalizika swala ya Ijumaa katika Msikiti Mushawar, Mwembeshauri Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiagana na mgeni wake Mfalme VI wa Morocco baada ya kumaliza swala ya Ijumaa.
Washauri wa Mfalme Mohamed VI wa Morocco wakitoka Msikiti wa mushawara baada ya kumalizika ibada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti huo.  Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.