Habari za Punde

Balozi Seif afika Mbuzini, ahani msiba wa Jaji Zuberi Juma Mzee

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Ubani wa Serikali kwa Mzee Khamis Vuai mwakilishi wa Familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar {ZEC} Marehemu Jaji Zubeir Juma Mzee aliyefariki Dunia jana na kuzikwa kijiji kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi “A”. 
 Baadhi ya Familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar marehemu Jaji Zubeir Juma Mzee wakipokea nasaha za pole kutoka kwa Balozi Seif hayupo pichani alipofika kutoa mkono wa pole.

Wanafamilia wa Marehemu Jaji Zubeir Juma Mzee wakitafakar jambo wakati wa kupokea mkono wa pole kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kijijini pao Mbuzini Wilaya ya Magharibi “A”.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.