Habari za Punde

Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ziarani Pemba kukagua miradi

 Mwenyekiti wa Kamati ya ,  Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Yussuf Hassan Iddi, akizungumza jambo la Uongozi wa Wizara ya Fedha Pemba, juu ya kuhakikisha Ujenzi unafanywa na Wizara hiyo wa kujenga Ofisi tatu za Serikali huko Gombani, hautokuwa kama Jengo la Wizara ya Fedha Tibirinzi Pemba,lililoanguka kabla ya kumalizika kujengwa wakati Mwenyekiti huyo na Kamati yake walipokuwa na ziara ya kikazi ya kutembelea Wizara hiyo Pemba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha , Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Yussuf Hassan Iddi (katikati) akipokea maelezo juu ya jengo la Wizara ya Fedha lililoko Tibirinzi Pemba, ambalo lilianguka kabla ya kukamilika ujenzi wake ambao ulikuwa ukijengwa na Mkandarasi Jackson Contractors kutoka Kenya.


 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya fedha ,Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakitembelea Kiwanja cha kufurahishia Watoto Tibirinzi wakati kamati hiyo ilipokuwa na ziara ya kikazi ya kutembelea Wizara ya Fedha Pemba.
 Mjumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, mheshimiwa Ussi Yahya , akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa ZSSF Pemba, Rashid Moh'd Abdalla, juu ya maendeleo ya Kiwanja hicho.
 Jengo la Wizara ya Fedha Pemba, lililoko Tibirinzi Pemba, ambalo lilijengwa na Mkandarasi Jackson Contractor kutoka Kenya na kuanguka kabla ya kukamilika na hivyo kuitia hasara Serikali kwa mamilion ya Fedha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Zanzibar, Abdulnassir  Ahmed Abdulrahaman, akitowa maelezo kwa Kamati ya Fedha , Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi juu ya kujenga Ofisi yake baada ya kulivunja

jengo ambalo wamepatiwa na Wizara ya Fedha Pemba, huko Mkungu malofa ChakeChake

Foundation ya Jengo la Ofisi tatu za Serikali zitakazojengwa huko Gombani Pemba, ambalo kamati ya fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi ilitembelea kuona maendeleo yake.

Picha na Bakar Mussa-Pemba,

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.