Habari za Punde

Nafasi za kazi Maktaba Kuu

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi ya kazi kwa ajili ya Maktaba Kuu ya Zanzibar kama ifuatavyo:-
1. Mkutubi Msaidizi Daraja la III (ZPSE – 03) “Nafasi 5” - Pemba na “Nafasi 2” - Unguja
Sifa za Waombaji:


• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Ukutubi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Majukumu: (Muombaji awe na uwezo wa kufanya kazi zifuatazo:-
• Kuandaa na kutunza kumbukumbu kwa njia mbali mbali ikiwemo Kompyuta.
• Kutayarisha vitabu hadi kufikiwa hatua ya kutumika na msomaji.
• Kusimamia program mbali mbali zinazoanzishwa.
• Kushajihisha jamii kuwa na matumizi ya maktaba.
• Kuazimisha na kupokea vitabu vilivyorejeshwa.
• Kupanga vitabu katika safu zake (Shelfs)


Jinsi ya Kuomba:

• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.


• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 18 Novemba, 2016 wakati wa saa za kazi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.