Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Shamata Shaame Khamis akiikariri hati ya kiapo kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja,(kulia)Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mihayo Juma Nhunga,akiikariri hati ya kiapo kabla ya kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja,(kushoto)Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe,Shadia Mohamed Suleiman,[Picha na Ikulu.]10/11/2016.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe,Saidi Hassan Said (kulia) akiwa na Washauri wa Rais wa Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mihayo Juma Nhunga, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Shamata Shaame Khamis katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe,Shadia Mohamed Suleiman, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali baada ya kuwaapisha Naibu Mawaziri katika Wizara mbali mbali hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.
STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 10.11.2016
![---](file:///C:/Users/user/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image004.gif)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Manaibu Waziri wapya ambao aliwateuwa
hivi karibuni kushika nyadhifa katika Wizara mbali mbali za Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Walioapishwa ni Mihayo
Juma Nhunga kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Shamata
Shaame Khamis, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa
na Idara Maalum za SMZ na Shadya Mohamed Suleiman, kuwa Naibu Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto.
Hafla ya kuwaapisha viongozi
hao ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi hao
ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa
Rais Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali
za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheri.
Wengine ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Maudline Castico, Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya
Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar, Wakuu wa
Vikosi vya SMZ na viongozi wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment