Habari za Punde

Wakulima wa mwani Pemba: Endeleeni na uzalishaji


 Na Salmin Juma Pemba

Wakulima wa mwani wilaya ya Micheweni wametakiwa kuendelea kuzalisha zao hilo licha ya changamoto ya bei kutoka kwa makampuni yanayonunua zao hilo.

Wito huo umetolewa na katibu tawala wilaya hiyo Hamad Omar Small wakati akiuzungumza na wandishi wa habari ofisi kwake jana .

Amesema serikali itambua bei ndogo ya zao na kwamba serikali itaendelea kuyashaiwishi makampuni yanayonunua zao hilo ili kuweza kuongeza bei ya mwani .

Aidha smaall amewapongeza akinamama wa wilaya hiyo kutokana na juhudi walizianzisha za kujikomboa na umaskini kwa kuwapatia taaluma zaidi .

Licha ya kuwa Zanzibar ni nchi ya tatu duniani inayasafirisha kwa wingi sokoni zao hilo ikitanguliwa na Uphilipino na Indonesia lakini bado wazalishaji wa zao hilo karibia ya wote wamekua wakilalamikia bei duni ya uuzaji wake tofauti na ugumu katika  uzalishaji wake, ambapo wanasema hali hiyo huwakwaza na kuvunjika moyo katika uzalishaji wa zao hilo.

Bei ya zao hilo kwa kilo ni baina ya shilingi 700=/, 600=/ na imewahi kushuka hadi kufikia shilingi 300=/ 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.