Habari za Punde

Zao hili ni mbadala wa Karafuu

Na Abdi Suleiman, PEMBA.


KATIKA karne ya 19 zanzibar ilikuwa nchini ya Utawala wa Oman, mwaka 1829 kazi ya kuanzisha mashamba ya mikarafuu ikaanz akwa kutumia watumwa kutoka bara.

Mwaka 1830 Zanzibar ilikuwa inaongoza kwa kilimo cha Karafuu, kupelekea haja ya kuongozeka kwa watumwa kutumika katika kilimo hicho.

Kutokana na hali hiyo watumwa waliweza kufikia asilimia 90% ya wakaazi wote wa Zanzibar kwa kipindi hicho, Sayyid Said aliona nafasi kubwa biashara ya Karafuu kwa ajili ya soko la Uhindi na kwengineko.

Biashara hiyo ikabadilisha uso wa mji wa Zanzibar wa karne ya 19, uliowahi kuwa kijiji kikubwa cha vibanda kando ya boma lililojengwa na Oman kama kizuizi dhidi ya Wareno.

Kutokana na kitabu cha historia, mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyengine mbali mbali duniani.

Miche ya mkarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Mauritius mwaka 1818, miti hii imestawi zaidi Visiwani Unguja na Pemba, ambavyo vinatoa asilimia 80 ya karafuu zinazohitajika duniani.

Zao hilo ni muhimu sana kwa Zanzibar, kwani ndio utu wa mgongo wa taifa, hivyo wakulima na wananchi wanapaswa kulithamini sana kwa kuacha kulifanyia udanganyifu.

Wananchi wengi wa Unguja na Pemba wamekuwa wakitegemea zao hilo, hivyo haipendezi sasa kulianza kuliharibu kwa kufanya udanganyifu.

Katika msimu wa 2015/2016 ZSTC lilinunua jumla ya Tania 5,745 za karafuu, zenye thamani ya shilingi bilioni 80.5 kwa wakulima Unguja na Pemba.

Katika msimu huo tani 313 zilizonunuliwa Unguja zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 4.3 na Pemba tani 5432 zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 76.2, tani 5,500 zilikadiriwa kununua Unguja tani 217 na Pemba tani 5283.

Hii yote ni kuwafanya wafanya wakulima wa zao hilo kuwa nao karibu ili kulipa hadhi na thamani zao hilo la karafuu ambalo ndio utu wa mgongo wa taifa.

Kwa muda mrefu ZSTC limekuwa likitegemea kilimo kimoja tu cha zao la Karafuu, jambo ambalo ndio utu wa mgogo wa taifa la wazazibari.

Kuwepo kwa mbinu za kuanzia vilimo vyengine ambavyo vitakuwa mbadala wa zao la Karafu ni jambo la kujivunia na lakufurahisha kwani sasa wakulima wengi watajikita katika kilimo hicho.

ZSCT sasa linakusudia kuanzisha kilimo cha miti ya Milangilangi na Miwardi, baada ya kutegemea zao moja la karafuu kwa uzalishaji wake.

Kilimo hichi kimeonekana kuwa na tija zaidi, kulingana na mazao mengine ambayo yanazalishwa na shirika hilo, ikiwemo Michaichai, Mrihani, mafuta ya Makonyo na Karafuu.

Bwana shamba wa shamba la Viungo la ZSTC lililoko Mtakata Wawi Chake Chake Pemba, Mkubwa Khamis Mohamed, alisema mafuta ya milangilangi ni ghali sana duniani.

Umaarufu wa Mti wa Mlangilangi umeanza kujitokeza, katika nchi za Madagascar, Commoro na  Ecuador ambako inaoteshwa kwa wingi kwa ajili ya uzalishaji mafuta, bei yake Euro 200 kwa kilo (EXTRA FINE GRADE) sawa na shilingi 480,000/= za Tanzania.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia shirika la ZSTC limejipanga kuanzisha kilimo cha Miwardi na Milangilangi, ili kutotegemea zao moja la karafuu, ambalo wazalishaji wake duniani wamekuwa ni wengi na kusababisha ushindani mkubwa wa biashara.

Visiwani Zanzibar miti hii haingizi kipato chochote, bali Miwardi hulimwa kwa matumizi madogo madogo, Mlangilangi unafahamika zaidi ni mti wa porini na mara nyingi inatumika kwa matumizi ya majenzi”alisema.

Lengo la ZSTC ni kuwa na mazao zaidi ya moja, yanayoweza kuuzwa nje ya nchi kwa bei kubwa zaidi, wakulima waweze kujiajiri zaidi kwa kuzalisha mazao mengi ya biashara baada ya kutegemea mazao waliyoyazoeya.

Hapa tutaweza kuzitumia na kuzitunza rasilimali zetu tulizonazo zanzibar, Zanzibar imekuwa na rasilimali nyingi sana kwa muda mrefu sana, huku zikiwa na faida kubwa nyingi.

ZSTC tayari limeshaanzisha maandalizi ya miti hiyo, hekta moja ya miti ya Milangilangi, yenye uwezo wa kuzaa Mauwa kuanzia miaka miwili mpaka mitatu, pamoja na hekta moja na nusu ya Miwardi katika Shamba lake la Mtakata kwa ajili ya majaribio.

Baada ya utafiti wa bei, shirika la ZSTC litapeleka mradi huu kwa Wakulima, pamoja na vikundi vya Ushirika na kuwahamasisha kwa kuwapatia miche, Vipeperushi pamoja na mafunzo ili kuwawezesha kuanzisha kilimo hicho.

Kama ilivyo kwa miti mengine mafuta ya miti hiyo hutengenezewa manukato mbali mbali, pamoja na matibabu ya maradhi mbali mbali ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi.

Wakulima wa zao la karafuu Zanzibar, wameipongeza Serikali kwa ubunifu wake wa kuanzisha mazo mbala ya karafuu, yatakayoweza kuinuwa uchumi wa nchi.

Mwinyi Rashid Mwinyi mkulima wa karafuu Mahonda, Wilaya ya Kasakazini “B” Mkoa wa kaskazini Unguja, alisema jambo hilo ni zuri, ikiwa mazao hayo yatakuwa na tija kwa wananchi na wakulima kwa ujumla.

Kuanzishwa kwa kilimo hicho kitaweza kuwafanya vijana, 
kujikita kwenye vilimo na kuachaku kukaa vibarazani na kutumia madawa ya kulevya, pamoja na kuzurura ovyo ovyo mitaani.

“sisi huku Wilaya ya Kaskazini B tutanyo maeneo mengi makubwa, kama vile mahonda, Mtalin, kinduni na mengine mengi, hata kuweza kuingoa minazi na miembe iliyokuwa imeshazeeka, ili kulima kilimo hicho”alisema.

Salum Suleiman Said mkaazi wa Mbuguwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, alisema kuanzishwa kwa zao hilo litaweza kuongeza ajira kwa vijana nchini.

Katika kipindi hiki kilimo cha mikarafuu kimeongezeka, hivyo kuanzishwa kwa kilimo cha Milangilangi na Miwardi kitawafanya baadhi ya wakulima kujikita katika kilimo hicho, kwani hata hiyo mikarafuu imekuwa ni vigumu kukubali kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“baadhi ya maeneo kilimo hiki sasa ni vigumu kukubali kuota, lakini tukiingia katika kilimo kengine kinaeza kukubali kama ilivyokuwa mikarafuu kipindi cha zamani”alisema.

Hata hivyo aliyomba serikali kufanya utafiti kwa kina juu ya kilimo hicho, kabla ya kukishusha kwa wakulima kuweza kulima pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima.

Kombo Juma Khamis Mkulima wa zao la Karafuu Mtambwe Nyali, alisema ni mipango mizuri ya serikali kuanzisha kilimo chengine, ili kuweza kupata kipato kikubw akama ilivyo zao la Karafuu.

Alisema zao la karafuu sasa hivi limekuwa likivamiwa na wakulima wengi, huku baadhi ya wakulima wakishindwa kufuata taratibu na ujuzi wa upandaji wa timu hiyo ya mikarafuu.

Miti ya Milangi langi na Miwardi itaweza kulimwa kwa nguvu hadi vijana, wataweza kujishirikisha katika shuhuli za kilimo ili kuweza kupata fedha.

ZSTC imetoa mikopo ya fedha taslim, kwa Wakulima na wanaokodi Mikarafuu kwa hatua za awali za uchumaji karafuu, pamoja na ununuzi wa majamvi ya kuanikia mwaka 2015/2016 jumla ya wakulima 126 Unguja na Pemba, wamekopeshwa shilingi 342,300,000/= zilizorudishwa shilingi 292,030,000/= na kubakia deni la shilingi 50,270,000/=.

Unguja Wilaya zilizopatiwa mikopo ni Kaskazini A wakulima 13 walikopa shilingi 14,300,000/= na walilipa shilingi 40,800,000/=, Kaskazini B wakulima 20 walikopa shilingi 50,400,000/= walilipa shilingi 38,100,000/=, Wilaya ya Kati wakulima 6 walikopa shilingi 22,000,000/= walilipa shilingi 16,900,000/=, Magharibi wakulima 4 walikopa shilingi 6,100,000/= walilipa shilingi 5,850,000/= jumla ya wakulima 43 walikopeshwa kiasi cha shilingi 119,800,000/=, huku wakilipa shilingi 101,650,000/= na kubakia deni la shilingi 18,150,000/=.

Pemba Wilaya zilizopatiwa mikopo ni Wete wakulima 28 walikopa shilingi 79,500,000/= na wamelipa shilingi 64,4800,000/=, Chake Chake wakulima 20 walikopa shilingi 57,000,000/= na kulipa shilingi 51,600,000/=, Micheweni wakulima 28 walikopa shilingi 47,000,000/= na wamelipa shilingi 36,000,000/=, Mkoani wakulima 17 walikopa shilingi 39,000,000/=  na wamelipa shilingi 39, 000,000/=, huku jumla wakulima 83 wamekopa shilingi 222,500,000/= wamelipa 191,080,000/= na kubakia shilingi 31,420,000/=.

EMAIL:abdisuleiman33@gmail.com.




SIMU:0718968355

1 comment:

  1. mkarafuu kwa ndani ya mwaka mmoja unaweza kuzalisha karafuu?.... angalia utangulizi wako hapo juu ambao hauna ukweli wowote.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.