Na Abdi Suleiman, PEMBA.
KATIKA karne ya 19 zanzibar ilikuwa nchini ya Utawala wa
Oman, mwaka 1829 kazi ya kuanzisha mashamba ya mikarafuu ikaanz akwa kutumia
watumwa kutoka bara.
Mwaka 1830 Zanzibar
ilikuwa inaongoza kwa kilimo cha Karafuu,
kupelekea haja ya kuongozeka kwa watumwa kutumika katika kilimo hicho.
Kutokana na hali hiyo watumwa waliweza kufikia asilimia 90%
ya wakaazi wote wa Zanzibar kwa kipindi hicho, Sayyid
Said aliona nafasi kubwa biashara ya Karafuu
kwa ajili ya soko la Uhindi na kwengineko.
Biashara hiyo ikabadilisha uso wa mji wa Zanzibar wa karne ya 19, uliowahi kuwa kijiji kikubwa cha vibanda kando ya boma
lililojengwa na Oman kama kizuizi dhidi ya Wareno.
Kutokana na kitabu cha historia,
mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu
nyengine mbali mbali duniani.
Miche ya mkarafuu ililetwa Zanzibar
kutoka Mauritius mwaka 1818, miti hii imestawi zaidi Visiwani Unguja na Pemba,
ambavyo vinatoa asilimia 80 ya karafuu zinazohitajika duniani.
Zao hilo ni muhimu sana kwa Zanzibar, kwani ndio utu
wa mgongo wa taifa, hivyo wakulima na wananchi wanapaswa kulithamini sana kwa
kuacha kulifanyia udanganyifu.
Wananchi wengi wa Unguja na Pemba wamekuwa
wakitegemea zao hilo, hivyo haipendezi sasa kulianza kuliharibu kwa kufanya udanganyifu.
Katika msimu wa 2015/2016 ZSTC lilinunua
jumla ya Tania 5,745 za karafuu, zenye thamani ya shilingi bilioni 80.5 kwa
wakulima Unguja na Pemba.
Katika msimu huo tani 313 zilizonunuliwa
Unguja zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 4.3 na Pemba tani 5432 zikiwa na thamani ya shilingi bilioni
76.2, tani 5,500 zilikadiriwa kununua Unguja tani 217 na Pemba tani 5283.
Hii yote ni kuwafanya wafanya
wakulima wa zao hilo kuwa nao karibu ili kulipa hadhi na thamani zao hilo la
karafuu ambalo ndio utu wa mgongo wa taifa.
Kwa muda mrefu ZSTC
limekuwa likitegemea kilimo kimoja tu cha zao la Karafuu, jambo ambalo ndio utu
wa mgogo wa taifa la wazazibari.
Kuwepo kwa mbinu za
kuanzia vilimo vyengine ambavyo vitakuwa mbadala wa zao la Karafu ni jambo la
kujivunia na lakufurahisha kwani sasa wakulima wengi watajikita katika kilimo
hicho.
ZSCT sasa linakusudia
kuanzisha kilimo cha miti ya Milangilangi na Miwardi, baada ya kutegemea zao
moja la karafuu kwa uzalishaji wake.
Kilimo hichi kimeonekana
kuwa na tija zaidi, kulingana na mazao mengine ambayo yanazalishwa na shirika
hilo, ikiwemo Michaichai, Mrihani, mafuta ya Makonyo na Karafuu.
Bwana shamba wa shamba la
Viungo la ZSTC lililoko Mtakata Wawi Chake Chake Pemba, Mkubwa Khamis Mohamed,
alisema mafuta ya milangilangi ni ghali sana duniani.
Umaarufu wa Mti wa Mlangilangi umeanza kujitokeza,
katika nchi za Madagascar, Commoro na
Ecuador ambako inaoteshwa kwa wingi kwa ajili ya uzalishaji mafuta, bei
yake Euro 200 kwa kilo (EXTRA FINE GRADE) sawa na shilingi 480,000/= za
Tanzania.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia shirika
la ZSTC limejipanga kuanzisha kilimo cha Miwardi na Milangilangi, ili
kutotegemea zao moja la karafuu, ambalo wazalishaji wake duniani wamekuwa ni
wengi na kusababisha ushindani mkubwa wa biashara.
“Visiwani Zanzibar miti hii haingizi kipato
chochote, bali Miwardi hulimwa kwa matumizi madogo madogo, Mlangilangi
unafahamika zaidi ni mti wa porini na mara nyingi inatumika kwa matumizi ya
majenzi”alisema.
Lengo la ZSTC ni kuwa na mazao zaidi ya moja,
yanayoweza kuuzwa nje ya nchi kwa bei kubwa zaidi, wakulima waweze kujiajiri
zaidi kwa kuzalisha mazao mengi ya biashara baada ya kutegemea mazao
waliyoyazoeya.
Hapa tutaweza kuzitumia na kuzitunza rasilimali zetu
tulizonazo zanzibar, Zanzibar imekuwa na rasilimali nyingi sana kwa muda mrefu
sana, huku zikiwa na faida kubwa nyingi.
ZSTC tayari limeshaanzisha maandalizi ya miti hiyo, hekta
moja ya miti ya Milangilangi, yenye uwezo wa kuzaa Mauwa kuanzia miaka miwili
mpaka mitatu, pamoja na hekta moja na nusu ya Miwardi katika Shamba lake la
Mtakata kwa ajili ya majaribio.

Kama ilivyo kwa miti mengine mafuta ya miti hiyo
hutengenezewa manukato mbali mbali, pamoja na matibabu ya maradhi mbali mbali
ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi.
Wakulima wa zao la karafuu Zanzibar, wameipongeza
Serikali kwa ubunifu wake wa kuanzisha mazo mbala ya karafuu, yatakayoweza
kuinuwa uchumi wa nchi.
Mwinyi Rashid Mwinyi mkulima wa karafuu Mahonda,
Wilaya ya Kasakazini “B” Mkoa wa kaskazini Unguja, alisema jambo hilo ni zuri,
ikiwa mazao hayo yatakuwa na tija kwa wananchi na wakulima kwa ujumla.
Kuanzishwa kwa kilimo hicho kitaweza kuwafanya
vijana,
kujikita kwenye vilimo na kuachaku kukaa vibarazani na kutumia madawa
ya kulevya, pamoja na kuzurura ovyo ovyo mitaani.
“sisi huku Wilaya ya Kaskazini B tutanyo maeneo
mengi makubwa, kama vile mahonda, Mtalin, kinduni na mengine mengi, hata kuweza
kuingoa minazi na miembe iliyokuwa imeshazeeka, ili kulima kilimo
hicho”alisema.
Salum Suleiman Said mkaazi wa Mbuguwani Wilaya ya
Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, alisema kuanzishwa kwa zao hilo litaweza kuongeza
ajira kwa vijana nchini.
Katika kipindi hiki kilimo cha mikarafuu
kimeongezeka, hivyo kuanzishwa kwa kilimo cha Milangilangi na Miwardi
kitawafanya baadhi ya wakulima kujikita katika kilimo hicho, kwani hata hiyo
mikarafuu imekuwa ni vigumu kukubali kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
“baadhi ya maeneo kilimo hiki sasa ni vigumu
kukubali kuota, lakini tukiingia katika kilimo kengine kinaeza kukubali kama
ilivyokuwa mikarafuu kipindi cha zamani”alisema.
Hata hivyo aliyomba serikali kufanya utafiti kwa
kina juu ya kilimo hicho, kabla ya kukishusha kwa wakulima kuweza kulima pamoja
na kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima.
Kombo Juma Khamis Mkulima wa zao la Karafuu Mtambwe
Nyali, alisema ni mipango mizuri ya serikali kuanzisha kilimo chengine, ili
kuweza kupata kipato kikubw akama ilivyo zao la Karafuu.
Alisema zao la karafuu sasa hivi limekuwa likivamiwa
na wakulima wengi, huku baadhi ya wakulima wakishindwa kufuata taratibu na
ujuzi wa upandaji wa timu hiyo ya mikarafuu.
Miti ya Milangi langi na Miwardi itaweza kulimwa kwa
nguvu hadi vijana, wataweza kujishirikisha katika shuhuli za kilimo ili kuweza
kupata fedha.
ZSTC imetoa mikopo ya fedha taslim, kwa Wakulima na
wanaokodi Mikarafuu kwa hatua za awali za uchumaji karafuu, pamoja na ununuzi
wa majamvi ya kuanikia mwaka 2015/2016 jumla ya wakulima 126 Unguja na Pemba,
wamekopeshwa shilingi 342,300,000/= zilizorudishwa shilingi 292,030,000/= na
kubakia deni la shilingi 50,270,000/=.

Pemba Wilaya zilizopatiwa
mikopo ni Wete wakulima 28 walikopa shilingi 79,500,000/= na wamelipa shilingi
64,4800,000/=, Chake Chake wakulima 20 walikopa shilingi 57,000,000/= na kulipa
shilingi 51,600,000/=, Micheweni wakulima 28 walikopa shilingi 47,000,000/= na
wamelipa shilingi 36,000,000/=, Mkoani wakulima 17 walikopa shilingi
39,000,000/= na wamelipa shilingi 39,
000,000/=, huku jumla wakulima 83 wamekopa shilingi 222,500,000/= wamelipa
191,080,000/= na kubakia shilingi 31,420,000/=.
EMAIL:abdisuleiman33@gmail.com.
SIMU:0718968355
mkarafuu kwa ndani ya mwaka mmoja unaweza kuzalisha karafuu?.... angalia utangulizi wako hapo juu ambao hauna ukweli wowote.
ReplyDelete