Habari za Punde

Wananchi watakiwa kuupokea utafiti mpya wa viashiria na matokeo ya Ukimwi kisiwani Pemba

Na Salmin Juma, Pemba

Wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kuwa tayari kuupokea utafiti mpya juu ya viashiria na matokeo ya ukimwi Tanzania wa mwaka 2016/17 utakaonza hivi karibuni kisiwani Pemba.

Nasaha hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Bi Mwanajuma Majid Abdalla huko katika ukumbi wa mikutano Gombani katika hafla ya mkutano wa wadau wa utafiti huo kisiwani Pemba.

Kupitia mkutano huo uliyojumuisha wadau mbali mbali wakiwamo waandishi wa habari walitakiwa kwa umoja wao wafikishe taarifa na elimu kwa jamii juu ya kuupokea utafiti huo ili jamii iweze kutoa taarifa sahihi kwenye utafiti huo muda utakapowadia na hiyo itakuwa kwa kaya ambazo zitachaguliwa kushiriki katika utafiti huo.

Mapema mwakilishi na mjumbe kutoka shirika la kimataifa lisilo la kiserekali ambalo ni mdau na mfadhili wa mradi huo ICAP bi Mihayo Lupamba amesema ni vyema wananchi wakauona umuhimu wa utafiti huo na kuupokea kwa mikono miwili kwani ni njia moja wapo ya kulisaidia taifa kuweza kupanga mipango yake ya maendeleo na hasa katika suala zima la afya na mapambano ya maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI humu nchini.

Amesema mradi huo utakuwa na utafiti mpana zaidi kwani hautaangalia tu maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI bali utakwenda mbali zaidi kuona pia viashiria vya maradhi mengine mbali mbali katika jamii kama vile kaswende na homa ya ini ili kujuwa ukubwa wa matatizo hayo na hio itakuwa kwa kila rika ikijumuisha watoto wa kuanzia miaka 10 kujia juu.

Aidha amesema utafiti huo utakuwa katika ngazi za mikoa na wilaya na kuzitaja shehia nane zitakazoshiriki katika utafiti huo kwa upande wa Pemba kuwa ni Mtambwe kaskazini na Maziwani kwa wilaya ya Wete na kwa upande wa wilaya Micheweni amezitaja shehia za wingwi mapofu na maziwa ng'ombe aidha wilaya ya chake amesema shehia ya kilindi pekee ndio itakayowakilisha katika mpango huo na kwa mkoani shehia ya KP, Stahabu, Ng'ombeni  zitawakilisha eneo hilo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.