Na.Asia
Hakim MUM
Leo waislam
wote duniani wanaadhimisha uzao wa Kiongozi wa Dini tukufu ya kiislam Mtume
Muhammad (S.A.W) hakuna budi angalau tukajikumbusha historia ya mtume japokwa
ufupi.
Kutoa
historia katika makala hii haina maana kuwa waislamu hawaijui historia ya Mtume,
au muandishi anajua sana kuhusu hili.
Bali ni vyema kukumbushana pindi nafasi inapotokezea.
Kiukweli
unapo fuatilia historia ya Mtume (S.A.W)
kuna mazingatio makubwa hususan katika maisha ya kila siku ya Muislam.
Katika
makala hii itagusia kwa ufupi historia ya Mtume kutoka kuzaliwa hadi kufikia kupewa
utume.
Kuzaliwa Kwake.
Mtume Muhammad (S.A W) alizaliwa mwezi 11 Mfungo sita alfajiri ya kuamkia siku ya Jumatatu sawa na April 21
mwaka 571.ambayo ilinasibiana na tukio la ndovu na Mfalme Kisra(mwaka wa Tembo)
ambapo ilikuwa ni mwaka wa 40 wa utawala wa Kisra. (Muhammad Suleiman,
Najatul-Afham)
Ibn Saad na Musnad Ahmad akaeleza kuwa Kuzaliwa kwa mtume
Muhammad (S.A.W) mbora wa viumbe vyote kulikua na Nuru na baraka kubwa iliyo angaza duniani na
ilikuwa ni ishara ya ukombozi wa jamii zote.
Ambapo mama
yake Mtume (S.A.W) ameripotiwa akisema ‘wakati alipojifungua ulitoka mwaga
mkubwa na kuelekea katika maeneo ya Syria na kuenea katika eneo lote’’
Ambapo anaendelea kwa kusema Baada nuru hiyo
kuenea Masanamu mbali mbali yaliporomoka na utawala wa Kisra ukaanguka pamoja
na wachawi kupata fadhaa.
Ibn Hisham anaeleza kuwa baada ya babu yake Mtume (S.A.W) Bwana Abdul Mutallib kupata ishara
njema ya kuzaliwa mtoto, alimchukua mjukuu wake na kwenda nae hadi kwenye Al-kaaba kwa ajili ya
kumuombea , na baadae kumpa jina la `Muhammad` na baada ya siku saba
akamtahiri.
Furaha ya
kuzaliwa kwa Mtume ilienea kwa familia nzima kwani pia Ami yake Abu Lahab aliamua kumpatia mlezi Mtume Muhammad (S.A.W)
ambae alikuwa mtumwa wake.
Mlezi huyo
alikuwa Bibi Thuaiba ambae alikua ni mtu
wa pili kumnyonyesha Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya mama yake Mzazi Amina bint
wahab.
Pia Mtume
Muhammad (S.A.W) alinyonyeshwa na Bi Halima
ambae alimchukua kwa ajili ya kumlea jambo ambalo ilikuwa ni ada kwa waarabu
kuwapeleka watoto wao kulelewa sehemu za mbali ili waweze kuwa na Afya nzuri kutokana na hali
mbaya ya hewa iliyokuwepo Makka.(sahihi Al-Bukhari).
Kwa mnasaba
huo watoto waliweza kukuwa na afya nzuri na pia kujifunza lugha fasaha ya
kiarabu ambayo haikuchafuliwa na
uingiliwaji wa lugha nyengine.
Ishara njema
zilijitokeza mapema kwa Mtume Muhammad (S.A.W) tokea wakati wa kulelewa na Bi
Halima yaliyojitokeza kutokana na
mabadiliko ya kiuchumi na maeneo mengine, mama huyu aliweza kunyonyesha watoto wengi kutokana na kujaa kwa maziwa na
hata ngamia wao aliyekuwa mgonjwa aliweza kutoa maziwa mengi.(zadul-maad uk
1/19)
Kutokana na
bahati nzuri zilizojitokeza katika kumlea mtoto huyo Bi Halima alimuomba mzazi
wake amuengezee muda wa kukaa na mtoto
huyo ili aendelee kupata kheri zake.
Abu Nuaim
katika kitabu chake cha dalailun Annubuwah anasema, mtume Muhammad (S.A.W)
Aliendelea kukaa na Bi Halima hadi alipofikia umri wa miaka minne.
imeoneshwa katika sahihi muslim kuwa alishuka
Malaika Jibril na kumfanyia upasuaji wa kifua na kuutoa moyo wake na kuuosha
katika maji ya Zam zam na baadae ukarejeshwa mahali pake.
Palikuwa na
watoto walioweza kuliona tukio hilo na kwenda kumwambia mlezi wake, ambae
alipatwa na wasiwasi na kuamua kumrejesha nyumbani kwao Makka.
Baada ya
kurudishwa kwa mama yake mzazi Mtume Muhammad (S.A.W) aliishi na mama yake hadi
umri wa miaka 6 ambapo mama yake alifriki dunia na kuzikwa katika kijiji cha
Abwa kinacho pakana kati ya Makka na Madina baada ya kuugua.( Ibnu Hisham)
1/168
Baada ya
hapo Mtume (S.A.W) alirudishwa kwa Babu yake Abdul Mutallib Huko Makka ambako aliishi nae kwa mapenzi makubwa zaidi kuliko watoto wake wote .
Ibni Hisham
anaeleza kuwa kwa mapenzi aliyokuwa nayo babu kwa mjukuu wake huyo ilifikia hadi kumruhusu Mtume (S.A.W)
kusali mbele katika Al kaaba wakati yeye pia akisali. Wakati watoto wake
walikuwa wakikaa nyuma ya baba yao kwa kumpa heshima.
Jambo hili hakuwahi kulifanya kwa mtoto wake
yoyote, na aliye jaribu kumuondoa mtume (.S.A.W) mbele alikatazwa na kuelezwa
kuwa ` mwacheni mjukuu wangu huyu
atakuja kushika nafasi kubwa`
Mzee Abdul Mutallib alionekana kumuamini sana
kijana wake kwani alikuwa akimshirikisha
katika mambo yake mengi kutokana alikuwa
akiridhishwa na vitendo vyake.
Wakati Mtume
Muhammad (SAW) alipofikia umri wa miaka 12 alikwenda katika safari ya bishara
na Ami yake Abu Talib katika nchi ya
Syria.
Walipofika
katika kijiji cha (Busra) ambacho kilikuepo katika maeneo ya Syria lakini
yakimilikiwa na Utawala wa Kiroma, katika kijiji hicho walikutana na Kasisi
mmoja wa Kikristo aliyeitwa Bahira(George)
Baada ya kumuona Kasisi huyo alimtambua Mtume (S.A.W) na kumtaka Ami yake arudi nae
huko Makka ili asije kudhuriwa na Watu wenye chuki dhidi yake. ( Ibni Hisham,
Talqih fuhum Ahlil-afham).
Wakati Abu
Talib alipotaka kujua ishara ya kijana yule kuwa ni Mtume wa Allah Bahira alijibu ‘’wakati mlipotokea katika
eneo hili miti yote na majabali yalianza kusujudu, jambo ambalo halijawahi
kutokea isipokuwa kwa mitume wa Allah (SW).
Pia nimemtambua Kijana huyu kuwa
atakuwa Mtume baada ya kuona muhuri wa Utume katika bega lake ambapo ishara hizi
nimeziona katika kitabu chetu’’ (At.Tirmidhi no 3620).
Baada ya
kupata maelezo hayo Abu Talib aliamua kumrudisha Mtume (S.A.W) Makka na yeye
akaendelea na safari.
Wakati Mtume
(S.A.W) akiendelea na maisha yake alijishughulisha na uchungaji wa wanyama
waliotoka katika ukoo wa Banii saad ambapo alikuwa akichunga kwa malipo.
Alipofikia
umri wa miaka 25 alikwenda Syria kwa ajili ya kufanya biashara za tajiri wake
Bi Khadija.
Ibn Ishaaq
anaeleza kuwa baada ya bibi Kadija kupata habari za kijana muaminifu katika
maneno na vitendo, mnyenyekevu na mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri. Alivutiwa nae
na kuamua kumuajiri awe mfanya biashara wake.
Mtume
Muhammad alikubali na kuanza kufanya biashara na katika safari yake ya kwanza
alifuatana na Maisara ambae alikuwa ni mtumwa wa bi Khadija.
Wakati Mtume
Muhammad (S.A.W) aliporejea kutoka safari ya biashara, mapato yaliongezeka mara
dufu na kumfanya Bi khadija kuzidi kuvutiwa nae. Sio hilo tu lakini hata
Maisara mwenyewe alieleza utofauti aliokuwa nao Mtume Muhammad (S.A.W) ambapo
alidiriki kununua vyakula vya bei rahisi ili asimtie hasara tajiri yake.
Pia katika
sahihi bukhari (2262) imeelezwa kuwa Baada ya bi khadija kuzielewa kwa undani tabia halisi na alivutiwa nae na alihisi wazi huyo ndiye aina ya Mume ambae alikuwa
anamuhitaji katika maisha yake, kwani yeye tayari aliuwa mtu mzima aliye wahi
kuolewa na kuzaa hivyo maisha ya ndoa alikua anayajua. Kwani wanaume wengi
walitaka kumuoa lakini alikataa.
Alifanya
haraka kumtuma rafiki yake Nafisa amueleze mtume (S.A.W)kuwa anataka afunge nae
ndoa, nae alifanya haraka kwenda kumueleza.
Mtume
(S.A.W) alikubali na alimtuma ami yake kwenda kutoa posa na haraka ndoa
ikafungwa wa mahari ya Ngamia ishirini.alibahatika kuzaa nae watoto sita kati ya
watoto saba.
Unapoelezea
historia ya Mtume (S,A.W) huwezi kusahau tokeo la uarabati Al-kaaba ambapo kwa kipindi hicho mtume (S.A.W) alikuwa na umri wa miaka 35 ambapo kila kabila
lilitaka kupata nafasi ya kujenga, baada ya mabishano ndipo likatoka wazo kuwa
atakae ingia ndani kwa muda huo kutoka nje ndie atakae toa maamuzi ya nani
abebe Jiwe jeusi.
Ghafla
alitokea Mtume (S.A.W) na wote walimkubali atoe suluhisho nae aliamuru kila
kabila litoe mtu mmoja kwa ajili ya kubela jiwe hilo. Ambapo alitandika kilemba
chake na kila kabila kuchukua ncha moja na yeye akachukua ilobaki, na makabila
yote yakawa yameshiriki katika ukarabati huo.(ibn hisham)
Pia katika
sahihi Albuhari imeelezwa kuwa Wakati alipokaribia miaka 40 Ilikuwa ni desturi
ya Mtume Muhammad (S.A.W) kujitenga kwa masaa adhaa akitafakari juu ya uumbaji
wa Allah (SW), pia huko alikuwa akifanya ibada mbali mbali na kuchukia ibada za
kushirikina.
Katika
sehemu ziliuwa maarufu kutembelea ilikuwa ni Mlima nuur na pango la hira ambapo
katika pangohilo ndipo alipopewa utume.
Pia katika
kipindi hicho mtumw (s.a.w) alikuwa akipata ilham kwa kuota mambo ambayo
yalikuwa yanatokea kweli. (Ibnu Hisham)
Wakati
alipotimia umri wa miaka arubainikama ilivyo kawaida kwa mitume wengine Mtume
Muhammad (S.A.W) aliabidhiwa juumu la kueneza nenola Allah (SW)kwa walimwengu
wote.
Na wahay wa kwanza kumshukia ulikuwa ni maneno matakatifu ya kuran. Wamekubaliana wana vyuoni kuwa siku halisi
aliyo pewa utume mtume Muhammad (S.A.W)
ilikuwa ni siku ya jumatatu mwezi 21 ramadhan ambayo ni sawa na Agosti 10 mwaka
610 C.E.
Hapo ndipo zikashushwa aya tano za kwanza kwa
mtume (S.A.W)ambazo zinatilia mkazo jambo la kutafuta elimu.
Hii ni
kuonesha kuwa ni kwa iasi gani dini hii ya Uislamu inavyo thamini mwenye kujua
mambo.na ndio maana Alla (SW) akawarahisishia pepo njia ya kwenda peponi wale
wanao tafuta elimu.
Ukija katika
maisha halisi ya jamii za sasa kuna baadhi ya watu kama kwamba hawajui kuwa
kusoma ni amri.kiasi kwamba wanafikia hatua kuufanya udhaifu wao ni hoja ya
kubishana juu ya jambo Fulani.
Mtu anafikia
hatua ya kusema `hata kama sijasoma laini kwa hili hunidanganyi` msemo huu ni
silaha ya wasiokubali kubadilika kwa kutojua lakini pia kutotaka kusoma.
Pia kuna watu wanao soma upande mmoja wa elimu na
kubeza upande mwengne wa elimu kwa kisingizio tu cha kuona upande huo hauna
maana.
Muhadhiri wa
Mkuu wa Kitivo cha Masomo ya uislamu kutoka Chuo Kikuu Cha Waislamu Cha
Morogoro Abdi Kassim Jiba anaeleza kuwa kufanya hivyo ni uwelewa mbaya wa
makusudo ya aya tano za kwanza zinazoonesha umuhmu na ulazma wa kusoma kwa
waislamu , kwanii kur- ani imeeleza wazi namna mtu anavyotakiwa kuwa makini
katka kuelewa dhana ya kusoma.
‘’hebu
chukulia mfano mdogo tu wa teknolojia ya anga na masomo ya sayansi wakati
kurani tukufu inashuka yalielezwa lakini swali la kujiuliza teknolojia ya karne
ya saba na sasa ni sawa hayo yamekuja kwa kusoma’’ anaeleza Jiba.
Pia
anaendelea kueleza kuwa kuisoma dini ni muhimu kwani bila ya kusoma hata ibada
zitakuwa na mushkeli. Kwa mujibu wa jiba anaeleza Tatizo hilo
linakuja kutokana na mfumo wa elimu hauwapi fursa wanafunzi wazazi na jamii kwa
ujumla nafasi ya kusoma na kuelewa dhana ya ``soma kwa jna la mola wako
aliiyeumba`` lakin kama llingejulikana hiya yote yasinge tokea.
Mkuu huyo
anatoa suluhsho katika makala hii ambapo anasema ni kuwaandaa walimu ambao
wataweza kuelimisha kizazi chote juu ya umuhimu wa elimu katika Nyanja zote za
maisha , lakini jamii kutaka hasa kwa moyo mmoja kujua na kutekeleza
yaliyomokatika elimu kivitendo.
Akitolea
mifano mbali mbali mkuu huyo ameitaja aya ya pili akisema huwezi kujua kama
binaadamu kaumbwa kwa tone la manii bila kufanya uchunguzi na uchunguz ni
sayansi, kurani imeeleza kila kitu lakini huwezi kuelewa bila ya kuwa mdadisi na
msomi.
Na ndio maana mwanaadamu akaumbwa kuwa iongozi
hapa duniani wa kuitawala dunia, lakini yote yanafanikiwa kwa kuelewa majukumu yote.
No comments:
Post a Comment