Kampuni ya Pennyroyal (Gibraltar)
Limited ina furaha kubwa kuutangazia umma kupitia vyombo vya habari kwamba, imesaini
Mkataba wa muda mrefu wa Uhandisi, Ujenzi na Manunuzi (ECP Agreement) na
Kampuni ya MCC Overseas Ltd (MCCO)” kutoka China kujenga mradi wa Pennyroyal wa
“Zanzibar Amber Resort”.
Sherehe hizi za
utiaji saini zilifanyika leo tarehe 14 Disemba 2016 katika Hoteli ya Park
Hayatt, Mji wa Mawe Zanzibar. Mkataba
huo ambao una gharama/thamani ya dola za kimarekani milioni 330. Kupitia Mkataba huo, Kampuni ya MCCO itakuwa
na jukumu la kuwa Mkandarasi wa mradi wa “Amber Resort” amabao watajenga villa
za kifahari, majengo ya makaazi (apartments), hoteli 5 kubwa zenye hadhi ya
nyota tano, marina, visiwa vya kifahari, kiwanja kikubwa cha kimataifa cha
mchezo wa golf na huduma zinazoendana na mji wa kitalii. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo inatarajiwa
kuanza katika kipindi kifupi kijacho na kumalizika mwaka 2020.
Ujenzi wa mji huu wa kitalii ambao
unakusudiwa kutekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa hekta 411 katika mwambao wa
bahari ya kijiji cha Matemwe, Kaskazini Mashariki ya Kisiwa cha Zanzibar,
utachangia sana jitihada za serikali za kuleta mabadiliko ya kiuchumi hususan
katika sekta ya utalii na uwekezaji wa nyumba za biashara (real estate
development).
Mradi huu utatekelezwa kwa
kutumia teknolojia ya kisasa, vyombo, mashine na utaalamu wa hali ya juu ambao
utazingatia kwa makini uhifadhi wa mazingira kwa kufuata taratibu na miongozo
iliyowekwa ya serikali na ile ya kimataifa ya kulinda mazingira ya ardhi na
bahari na masharti ya Hati ya Tathmini ya Athari za Kimazingira (Environmental
Impact Assessment – E.I.A) iliyotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa
mradi huu. Aidha, maisha ya jamii
katika vijiji vinavyozunguka mradi huu yataimarika kwa kiwango kikubwa.
Tukio hili limeweka historia kwa
kampuni binafsi ya Pennyroyal kuithibitishia dunia kuwa uwekezaji mkubwa kama
huu utaleta mafanikio makubwa yatakayoibadilisha Zanzibar katika ramani ya
dunia kwa kuwa na utalii wenye hadhi ya juu, maendeleo ya uwekezaji wa ujenzi
wa nyumba za kibiashara na kuifanya Zanzibar kuwa eneo vutivu duniani.
Mradi huu utakapomalizika utaongoza
kwa miradi ya sekta binafsi kwa kutoa ajira kwa takriban watu 2000 ambao
watafanya kazi katika hoteli tano kubwa zenye hadhi ya nyota tano, ajira katika
viwanja vyenye vya golf vyenye hadhi ya mashindano ya kimataifa, katika nyumba
zenye apartments 3500, villa za kifahari 1900, na katika visiwa na maeneo yanayotoa
huduma mbalimbali kama vile maduka, mabenki na huduma za kijamii.
Katika kusaidia jamii, Pennyroyal ina
mpango maalum (corporate social responsibility) wa kuwajenga uwezo wanavijiji
katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, mafunzo stadi, kilimo endelevu
na miradi mengine ya kuwafikia wananchi ya kunyanyua maendeleo ya kuchumi na
kupunguza umasikini
Mkataba huu na kampuni ya MCC Overseas
Ltd ya China, ambayo imo katika orodha ya kampuni 500 kubwa duniani, ni
kielelezo kikubwa cha urafiki wa kihistoria kati ya China na Tanzania. Ushiriki wa MCCO ni tija iliyo wazi kwa
Zanzibar kupata fursa ya kuongeza uzoefu na ubunifu katika ujenzi wa eneo kubwa
utakaotekelezwa na mmoja kati ya wakandarasi wakubwa duniani
No comments:
Post a Comment