Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbali mbali katika uzinduzi wa Matokeo
ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2015-16 Tanzania
jijini Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya
Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es
Salaam
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na wadau mbali mbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya
Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2015-16 Tanzania
jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Sensa ya
Watu na Takwimu za Jamii Sylivia Meku akielezea kwa wadau wa afya Matokeo ya Utafiti wa Afya
ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es
Salaam. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dr. Albina Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya
Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es
Salaam
Waziri
waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, WazeenaWatoto, Mh.
Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wadau mbali mbali wa Takwimu na Afya katika uzinduzi wa Matokeo
ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania
jijini Dar es Salaam leo (jana). (Pichana
Benjamin Sawe- Maelezo)
Na. Eliphace Marwa – Maelezo
SERIKALI imezindua ripoti ya utafiti wa afya ya
uzazi na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2015/16 mapema hii leo jijini
Dar es Salaam ikiwa ni awamu ya tatu katika ugonjwa wa malaria ambapo ripoti
imeonesha kupungua kwa vifo vya watoto wadogo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi ambaye
pia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy
Mwalimu ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuaanda ripoti iliyoonesha
Taifa kupiga hatua katika utoaji wa huduma ya mama na mtoto.
Waziri Ummy ameeleza kuwa ripoti hiyo itaisaidia
Wizara ya Afya na serikali kwa ujumla katika kutathmini na kufuatilia
utekelezaji wa mipango endelevu katika huduma za afya hapa nchini ili kuboresha
utoaji wa huduma ambazo ripoti imeonesha haikufanya vizuri kutokana na
changamoto mbalimbali ambazo ripoti imezibainisha.
“Ripoti hii imeonesha kuwa bado kuna changamoto
katika mimba za utotoni kwani zimeongezeka ukilinganisha na mwaka 2010
ambapo watoto 23 kati ya mia moja walipata mimba wakiwa na umri mdogo
ukilinganisha na sasa watoto 27 kati ya mia moja hupata mimba katika umri mdogo
hivyo kuna haja ya jamii kuelimishwa juu ya madhara ya mimba za utotoni”,
alisema Waziri Ummy.
Aliongeza kuwa kuna haja ya serikali kuangalia
upya sheria ya kuruhusu mwanafunzi kuendelea na masomo endapo akipata mimba
akiwa shuleni kwani kumzuia kuendelea na masomo ni kupoteza nguvu kazi ya taifa
na kuikwamisha serikali kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa iwapo huduma za afya zitaboreshwa
zitapelekea ukuaji wa uchumi kwasababu ya uwepo wa nguvu kazi ya uhakika na
kuongeza uzalishaji kwa Taifa.
“Wananchi wakiwa hawana afya ya kutosha na kuugua
mara kwa mara uchumi wa nchi yoyote Duniani hupungua kasi ya ukuaji kwa kuwa
rasilimali fedha ambazo zingeelekezwa kukuza sekta nyingine hupungua na hata
nguvu kazi kupungua” alisema Dkt. Chuwa.
Aidha Dkt. Chuwa aliongeza kuwa kwa mujibu wa
Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 inatamka kuwa yeyote atakaepotosha Takwimu hizi
kwa makusudi atachukuliwa hatua za
kisheria kupitia kifungu cha 37 cha
sheria hiyo.
Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa mwaka 1991-92
ulionyesha kuwa katika kila watoto 1000 wanaozaliwa hai, watoto 141 walikuwa
wakifariki kabla ya kufikia umri wa miaka mitano ila utafiti huu umebaini kuwa
ni watoto 67tu ndiyo wanaofariki kati ya watoto 1000.
No comments:
Post a Comment