Habari za Punde

Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Chafanya Mkutano Mkuu Wake wa Mwaka Mjini Zanzibar.

  Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Omar Said Shaaban akizungumza na wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa siku moja uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.

 Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee akiwasilisha mada ya mwenendo wa kesi za makosa ya jinai katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar uliofanyika  Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha wanasheria Zanzibar wakifuatilia Mkutano Mkuu wa mwaka wa siku moja katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
 Mwanasheria wa siku nyingi na mwanachama wa chama cha wanasheria Zanzibar Nassor Khamis akitoa mchango wake kwenye mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar Omar Said Shaaban akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika Mkutano Mkuu wa mwaka wa siku moja katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.