STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 5.2.2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewasisitiza vijana kuendelea kutambua
thamani ya Mapinduzi na wajibu wa kuyatetea na kuyalinda kwa kutambua kuwa ndio
mkobozi wa taifa letu na ndio chachu ya
maendeleo yanayoendelea kupatikana hivi sasa
Akitoa neno la shukran mara baada ya chakula alichowaandalia vijana walioshiriki katika halaiki kwenye sherehe za
maadhimisho Ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika huko
katika viwanja vya vya Makao Makuu ya KVZ kwa niaba ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji
Ussi Gavu alisema ni vyema kwa
vijana kuendelea kuwa na mbegu za kizalendo ili kuendelea kunawirisha dhama ya
Mapinduzi kwa miaka mingi zaidi ijayo
Alisema ushiriki wa vijana hao uliojaa furaha katika sherehe hizo umeendelea kumpa moyo na
matumaini makubwa Dk. Shein na hivyo anaamini kuwa kutaendelea ya kujenga
hamasa kwa kushiriki kwa wingi zaidi katika sherehe zijazo zinapofikia za
kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar kwa miaka ijayo.
Hata hivyo Dk. Shein alitoa pongezi maalum kwa vijana hao wa halaiki na
makundi mengine yaliyoweza kushiriki vyema
na kufanikisha sherehe hizo ambazo zilikuwa kubwa na za aina yake.
Mapema Katibu wa uhamasishaji wa Halaiki
Ali Mohamed Baraka SHASHA amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed kwa kuendeleza utaratibu wa kuyakutanisha makundi
mbali mbali kwa ajili ya kupongezana kutokana na kazi nzuri zinazofanyika
katika sherehe hizo.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zubeir Ali Maulid, Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji
Omar Kheir, na viongozi wengine wa serikali.
Mwandishi Yunus Sose. Idara ya
Mawasiliano (Ikulu)
No comments:
Post a Comment