Habari za Punde

Serikali kugawa vifaranga vya samaki kwa wakulima kuanzia Oktoba

Na Salmin Juma , Pemba

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inatarajia kugawa vifaranga vya samaki kwa wakulima ifikapo mwezi agosti mwaka huu.

Waziri wa kilimo uvuvi na mifugo Mh Hamad Rashid Moh’d amesema tayari Serikali imeshataayarisha nasari ya mazalio ya vifaranga hao na muda si mrefu vitagawanywa kwa wakulima .

Ameyasema hayo huko Ukumbi wa kilimo Weni Wete katika  mazungumzo na wakuu wa mikoa ,wilaya na maafisa wa ulinzi na usalama wakati akielezea  fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Zanzibar.

Waziri huyo amesema endapo wananchi watachangamkia fursa zilizopo wanaweza kuinua kipato chao cha uchumi kupitia kilimo hicho cha ufugaji wa samaki.

Hamad amedokeza kwamba Vifaranga vya samaki vipatavyo elfu nane tayari vimeshatayarishwa kugaiwa wakulima wa samaki Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.