Habari za Punde

Shamrashamra za siku ya Sheria ilivyoanza kuadhimishwa kisiwani Pemba

 WATENDAJI wa mahakama, maofisa wadhamini, wanasheria, watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria, waendesha mashitaka, viongozi wengine wa serikali na wanavikundi vya mazoezi, wakiwa katika matembezi maalumu, ikiwa ni shamra shamra za kuelekea siku ya sheria, ambapo matembezi hayo ya kilomita tatu, yameanzia Mahakamu kuu Pemba na kumalizia uwanja wa michezo Gombani Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 WANAVIKUNDI vya mazoezi kisiwani Pemba, wakiungana na wanasheria wengine kisiwani Pemba, kwenye matembezi maalumu ya kuadhimisha siku ya sheria, ambapo matembezi hayo, yalioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, yalianzia jengo la mahakamu kuu Chakechake na kumalizia uwanja wa michezo Gombani, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 VIONGOZI kadhaa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla mwenye jaketi nyongani, akinyoosha viungo, mara baada ya kumalizia matembezi ya kilomita tatu, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za kuelekea siku ya sheria dunia, ambayo itaadhamishwa Febuari 9, mwaka huu kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WANAVIKUNDI vya mazoezi, wanasheria na viongozi wa serikali, wakiwa kwenye mazoezi makali, mara baada ya kuamliza matembezi ya kilomita tatu yalioanzia mahakama kuu Chakechake na kumalizia uwanja wa michezo Gombani, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya siku ya sheria, ambayo itafikia kielele Febuari 9, mwaka huu kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WATENDAJI, wa mahakama, wateule wa rais, waendesha mashitaka na wanasheria wengine, wakikaza meno, katika mchezo wa kuvuta kamba, ingawa walibururwa na Polisi, mchezo huo ni sehemu ya shamra shamra za kuelekea kilele cha siku ya sheria, ambayo huadhimishwa kila Febuari 9 ya kila mwaka, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WASHINDI wa mchezo wa kuvuta kamba ambao  ni Jeshi la Polisi, waliowavuta watendaji wa mahakama, wateule wa rais, waendesha mashitaka na wanasheria wengine, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra kuelekea siku ya sheria duniani, ambapo inatarajiwa kuadhimishwa Febuari 9 mwaka huu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WAFANYAKAZI, wa mahakama kisiwani Pemba, walipowavuta wapiganaji wa jeshi la Polisi wanawake, kwa mchezo wa kuvuta kamba, uliofanyika uwanja wa Gombani ikiwa ni shamra shamra za kuelekea siku ya sheria hapo Febuari 9 mwaka huu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MRAJISI Mahakamu kuu Jimbo Pemba Hussein Makame Hussein akizungumza kwenye shamra shamra za kuelekea siku ya sheria, kwenye uwanja wa michezo Gombani Chakechake Pemba, ambapo kabla walifanya matembezi yalioanzia mahakama kuu na kuishia uwanjani hapo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza kwenye shamra shamra za kuelekea siku ya sheria, kwenye uwanja wa michezo Gombani Chakechake Pemba, ambapo kabla Mkuu huyo wa Mkoa aliongoza matembezi, yalioanzia mahakama kuu na kuishia uwanjani hapo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.