Habari za Punde

WorldRemit imeshuhudia ongezeko kubwa la shughuli za kutuma pesa nchini Tanzania

WorldRemit


VYOMBO VYA HABARI

WorldRemit imeshuhudia ongezeko kubwa la shughuli za kutuma pesa nchini Tanzania

Huduma hii dijitali ya kutuma pesa hufanya shughuli 10,000 za kipekee kila mwezi
DAR ES SALAAM, Tanzania, Tarehe 17 Februari, 2017/ -- Huduma dijitali ya kutuma pesa, WorldRemit (www.WorldRemit.com/en/Cameroon), inaimarisha huduma zake nchini Tanzania, ili kushughulikia mahitaji yanayoongezeka ya malipo ya papo hapo nchini, kutoka zaidi ya wananchi milioni 4 wanaoishi ng’ambo.
Sasa, WorldRemit inatangaza:
  • Idadi mpya ya shughuli 10,000 za kipekee zilizokamilishwa mwezi wa Desemba 2016 pekee;
  • Ongezeko la kila mwaka la 150% katika mwaka wa 2016, lililotokana na kuongezeka kwa haraka kwa akaunti za Pesa Rununu kuwa njia maarufu zaidi ya kupokea pesa.
Wateja wa WorldRemit wanaweza kutuma pesa nchini Tanzania kupitia Pesa Rununu kwa akaunti za Tigo Pesa, Vodacom M-Pesa na Zantel Ezy Pesa, na pia kuweka pesa kwenye benki na kuchukua pesa taslimu.
Watumaji wakuu wa pesa za kuingia Tanzania wanajumuisha wahamiaji wanaoishi Uingereza, Uswidi, Australia, Norwe na Kanada, miongoni mwa nchi nyingine.
Kupitia WorldRemit, watu wanaoishi katika zaidi ya nchi 50 wanaweza kutuma pesa papo hapo kwa njia salama kwenda kwa zaidi ya sehemu 140. WorldRemit, inayojulikana kama ‘WhatsApp ya Pesa’, imefanya shughuli ya kutuma pesa kuwa rahisi kama kutuma ujumbe.
Pesa zinazotumwa huchangia sana katika kukuza uchumi wa Tanzania - mwaka wa 2015, nchi hii ilipokea jumla ya milioni $390 kulingana na Banki ya Ulimwengu. Kiasi hiki ni takribani mara kumi zaidi ya kiasi kilichotumwa mwaka wa 2010.
Ismail Ahmed, mwanzilishi na Afisa Mkuu Mtendaji wa WorldRemit, anasema: “Ushirikiano wa huduma yetu ya Pesa Rununu, ikiwa pamoja na huduma zilizopo za kuweka pesa kwenye benki na kuchukua pesa taslimu, utawapa Watanzania chaguo nyingi zaidi. Hii itasababisha mabadiliko kutoka huduma ghali za kutuma pesa nje ya mtandao kupitia mawakala wa mitaani hadi huduma za kasi, za bei nafuu na salama za kutuma pesa kupitia mtandao".
Kwa sasa, wateja wa WorldRemit hufanya zaidi ya shughuli 580,000 za kutuma pesa kila mwezi.
Kusambazwa na APO kwa niaba ya WorldRemit.

Kwa maelezo zaidi:
media@Worldremit.com

Kuhusu WorldRemit:
WorldRemit (www.WorldRemit.com) inabadilisha jinsi watu wanavyotuma pesa.  

Ni rahisi –  fungua programu tu au utembelee tovuti –  hakuna kwenda kwa mawakala tena.

  • Shughuli za kutuma pesa katika nchi nyingi hukamilika papo hapo – tuma pesa jinsi unavyotuma ujumbe wa gumzo.
  • Njia zaidi za kupokea pesa (Pesa Rununu, hawala ya benki, pesa taslimu na vocha ya simu).
  • Inapatikana katika zaidi ya nchi 50 na zaidi ya sehemu 140.
  • Inatumiwa na Accel Partners na TCV – wawekezaji katika Facebook, Spotify, Netflix na Slack.

Makao makuu ya kimataifa ya WorldRemit yako jijini London, Uingereza; na ofisi za maeneo zipo nchini Marekani, Kanada, Afrika Kusini, Singapori, Ufilipino, Japani, Australia na Nyuzilandi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.