Habari za Punde

Kongamano la Baraza la Vijana wa Shehia ya Miembeni Zanzibar Kupinga Udhalilishashi wa Wanawake na Watoto Zanzibar.

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Dkt. Sira Ubwa Mwamboya akiwahutubia Vijana wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni Zanzibar katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Mwanamke Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 March. 
Mlezi wa Baraza la Vijana Miembeni Mhe Mgeni Hassan Juma akitowa nasaha zake wakati wa Kongamano hilo la Vijana wa Miembeni Zanzibar kupiga Vita Vitendo vya Uzalilishaji wa Wanawake na Watoto vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.


 Mratibu wa Kongamano Baraza la Vijana wa Miembeni kutoka Taasisi ya Wanasheria Wanawake Zanzibar ZAFELA Jamila Mahmoud akitowa maelezo wakati wa Kongamano hilo katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Mtoa Mada kutoka Jeshi la Polisi Kituo cha Nga'mbu Dawati la Wanawake na Watoto akitowa mada kuhusiana na vitendo vya uzalilishaji wanavyofanyiwa watoto na wanawake Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.