Habari za Punde

Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi Wanalalamikia Uvuvi Haramu Katika Bahari Yao na Kwenda Maeneo ya Mbali Kuvua.

Mwananchi Mvuvi swa Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya makampuni katika ukanda wao wa bahari ya nungwi kwa kutumia bunduki na mishare wakati wa uvuvi wao na kuwakimbiza samaki katika maeneo hayo na wao inawalazimu kwenda kuvua seheme ya mbali na eneo hilo kutokana na samaki kukimbilia maeneo mengine, wameitaka taasisi husika kulichunguza hili. ili mkuepusha uvuvi huo haramu katika pwani yao.
Mwananchi wa Kijiji cha nungwi Unguja akizungumza na waandishi wa habari kero yao kwa waandishi kutokana na kukithiri vitendo vya uvuvi haramu jua Serikali inapiga vita uvuvi huo bado kuna watu wanatumia bunduki na mishare katika uvuvi huo.Wao wameachana na uvuvi haramu wa kutumia nyavu za matundu madogo na kuendelea kuvua kwa uvuvi unaotakiwa na Serikali kwa kutumia nyavu za macho makubwa.  

Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi wakiwa katika eneo la ufukwe wa bahari hiyo wakati wakiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika ukanda huo wa pwani ya nungwi wakiwa katika kazi zao za kawaida.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.