Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche (kushoto) akikagua nyaraka toka kwa
Msimamizi wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited Bw. Godwin Mungere mapema leo hii
jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji
wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Msimamizi wa Kiwanda cha True
Bell (T) Limited Bw. Godwin Mungere (mwenye shati la njano) akionesha baadhi ya
vifungashio vya pombe kali aina ya kiroba mapema hii leo Jijini Dar es Salaam wakati
wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho
Serikali imepiga marufuku kutumika, kulia ni Mwanasheria toka Baraza la Taifa
la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche
Msimamizi wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited
Bw. Godwin Mungere akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mara baada
ya ukaguzi wa pombe kali aina viroba katika kiwanda chake cha True Bell (T)
Limited wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji
hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Msimamizi wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited Bw.
Godwin Mungere ambao ni watengenezaji wa pombe ya Viroba aina ya Bonanza
akionesha baadhi ya nyaraka kwa Afisa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Timoth Mgaya wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka
wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Mkaguzi wa Chakula toka TFDA Bw. John Nzila
akitoa maelekezo kwa Mmiliki wa Kiwanda cha Blue Nile Bw. Mohan ambao ni
watengenezaji wa pombe za kiroba aina ya Kitoko na Rivella wakati wa siku ya
pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali
imepiga marufuku kutumika
Mwanasheria toka Baraza la
Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akiwaonesha waandishi
wa habari pombe aina ya Kitoko inayotengenezwa na Kiwanda cha cha Blue Nile wakati
wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho
Serikali imepiga marufuku kutumika.
Picha
zote na Eliphace Marwa - Maelezo
Baadhi ya Maafisa wa Serikali wakiwa nje ya Kiwanda
cha Triple S kilichopo Wazo Mivumoni ambacho kinatengeneza pombe za viroba aina
ya Signal True kikiwa kimefungwa na wamiliki wake kutoonekana wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka
wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika
Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo
No comments:
Post a Comment