Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar Yatiliana Saini na Jamuhuri ya Watu wa Palestina Makubaliano ya Mapya ya Miaka Mitano.Katika Sekta ya Afya.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akitiliana saini na Balozi wa Palestina Nchini Tanzania Mhe.Hazem Shabat, ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya Afya Zanzibar kwa miaka mitano na Wizara ya Afya Zanzibar itapatiwa misaada ya kitaaluma kutoka Palestina, hafla hiyo ya utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo kibadilishana mikataba baada ya kusaini na Balozi wa Palestina Nchini Tanzania Hazem Shabat,hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar. 

Na.Ramadhani Ali Maelezo Zanzibar.
Wizara ya Afya imetiliana saini na Jamhuri ya watu wa Palestina makubaliano mapya ya mashirikiano ya miaka mitano ambapo Palestina itaipatia Wizara msaada wa mafunzo kwa madaktari na wafanyakazi wa kada nyengine.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alitia saini kwa niaba ya Wizara na Palestina iliwakilishwa na Balozi wa Nchi hiyo Tanzania Hazem Shabat.
Akizungumza katika shehere hiyo iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Waziri wa Afya alisema kupitia mashirikiano hayo mapya Palestina wameonyesha hamu kubwa ya kusaidia masuala ya taaluma kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Amesema Palestina imekuwa rafiki mkubwa wa Zanzibar lakini mashirikiano hayo mapya yatapanua wigo mpana zaidi wa missada yake ambayo itawanufaisha wananchi
Alisema kwa kuanzia madaktari kutoka Palestina  wataweka kambi ya matibabu ya maradhi mbali mbali Zanzibar kwa kushirikiana na madaktari wazalendo kuanzia mwezi Agasti mwaka huu.
Aliongeza kuwa Madaktari wa Zanzibar watapata fursa ya kwenda Palestina na wao kuja Zanzibar kwa lengo la kubadilisha uzoefu na kujifunza katika taaluma hiyo.
Naye Blozi wa Palestina nchini Tanzania Hazem Shabat alisema mashirikiano ya nchi yake na Tanzania yalianza tokea wakati wa Mwalimu Nyerere ambapo Madaktari bingwa kutoka Palestina walikuwa wakija kusaidia matibabu.
Alisema makubaliano mapya ya sasa ni kuzidi kuimarisha mashirikiano hayo na kuahidi kuwa nchi yake itaongeza ushirikiano katika sekta nyengine zikiwemo kilimo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.